Habari za Punde

*USHAURI WA WADAU WA SOKA KWA KOCHA WA YANGA KUELEKEA MCHEZO WA MARUDIANO NA AL-AHLY

TIMU ya soka ya Yanga, inaondoka leo usiku kuelekea Jijini Cairo Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Afrika na Al-Ahly, huku ikiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika mchezo huo wa marudiano.

Wakati Yanga wakiondoka leo mashabiki wa soka nchini bila kujadi itikadi zao hawakusita kugonga hodi katika ukurasa wa mtandao huu na kutoa maoni yao na ushauri kwa Yanga ili waweze kuibuka na ushindi na kuitangaza Tanzania katika medani ya soka na kuandika ukurasa mpya wa historia kwa waarabu hao ambao siku za nyuma wamekuwa na historia ya ubabe kwa timu za Tanzania.

Baadhi ya wadau wa soka wameshushwa na taarifa ya Shirikisho la Soka la Misri kuwa mchezo huo utachezwa bila mashabiki kutokana na sababu za kiusalama zaidi.

Kwa upande wa Viongozi wa Yanga wao wamesema kuwa utaratibu huo kwao utakuwa ni 'advantage' ahueni kutokuwa na mashabiki wa timu pinzani ambao huwa wanautaratibu wa kushangilia mwanzo wa hadi mwisho wa mchezo huku wakiwasha mafataki ya rangi muda wote jambo ambalo lingewachanganya zaidi wachezaji wa Yanga.

Lakini kwa upande wa Wadau wa soka nchini, wamesema kuwa mchezo huo kutokuwa na mashabiki pia itakuwa ni hatari kwa timu ya Yanga, kutokana na uzoefu wa Al-Ahly ambao mara nyingi wamekuwa wakicheza zaidi soka lao nje na ndani ya uwanja.

Akizungumza na mtandao huu, mmoja wa wadau wa soka, ambaye ni shabiki wa Simba aliyejitambulisha kwa jina la John Shauri, alisema kuwa miongoni mwa hujuma zinazoweza kufanywa na wapinzani wa Yanga ni Al-Ahly ni kucheza na Waamuzi wa mchezo huo kwa kujiamini kuwa hakuna watazamaji wala ushahidi kwa maamuzi ya ajabu yanayoweza kutolewa na waamuzi.

Aidha Shauri, aliwataka viongozi wa Yanga kuomba mchezo huo hata kama hautakuwa na watazamaji basi uweze kuonyeshwa live, ili watu waweze kuuona moja kwa moja na iwapo vitatokea vitendo vya uonevu Yanga waweze kudili mapema na kukata rufaa.

Wadau wengine walishauri kuwa ni bora Yanga wao wakaenda kucheza mchezo ule ule kama waliocheza wiki iliyopita bila kujali mbinu za wapinzani za kupooza mpira na hata ikiwezekana kuongeza speed ya mchezo zaidi ili kuwachanganya wapinzani na kutoruhusu mipira kuelea elea maeneo ya hatari ya 18 katika dakika zote za mchezo kwamba 'Beki hasifiwi'.

Yanga imetakiwa kuimarisha zaidi safu ya ukuta wake ili kuhimiri mikiki ya mashambulizi na kutobweteka na ushindi wa bao 1-0 la nyumbani.  Ili kusonga mbele Yanga inahitaji Droo ya aina yeyote ama ushindi wa namna yeyote na iwapo watashinda ama kudroo watakuwa wameondosha mashindanoni mabingwa hao watetezi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.