Kikosi cha timu ya Taifa 'Taifa Stars' kilichowakabili Wagambia jana.
Timu ya Soka ya Tanzania, Tiafa Star jana imelazimishwa sare ya bao 1-1 na wenyeji Brave Warriors ya Namibia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa jana usiku kwenye uwanja wa Sam Nujoma, Katutura- Windhoek Namibia.
Goli la Stars lilifungwa na Hamis Mcha, aliyeunganisha mpira wa kona na katika dakika ya 86 na dakika tisa baadaye wenyeji waliweza kusawazisha kupitia mcheszaji Nekundi Haleluya Panduleni, na kufanya mchezo huo kumalizika kwa timu hizo kufungana bao 1-1.
Matokeo hayo yamemnusuru kocha Ricardo Manentti na benchi zima la ufundi la Brave Warriors ambao wamekuwa na matokeo mabaya kwa michezo zaidi ya minne ya kimataifa waliokwishacheza.
No comments:
Post a Comment