Mvua zilizonyesha jijini Dar es Salaam, siku ya jana zilizotolewa tahadhali na Mamlaka ya hali ya hewa zimesababisha kujaa maji katika baadhi ya maeneo na nyumba za wakazi wa jijini.
Baadhi ya maeneo yaliyojaa maji ni pamoja na Hospitali ya Hospitali ya Halmashauri ya Kinondoni Sinza - Palestina, ambayo ilijaa maji kila kona na kusabisha wauguzi kuacha kazi na kupanda juu ya Meza na viti kukwepa maji hayo.
Maji hayo mengi yalikuwa ni machafu yaliyochanganyikana na maji kutoka katika mitaro na chemba za maji machafu.
Mmoja wa wagonjwa akiwa anangojea kupata huduma baada ya mvua hiyo kubwa kwisha.
Haya ni maji machafu ambayo yametapakaa kila sehemu ya hospitali
Kushoto ni Mgonjwa akiwa amelala juu ya Benchi ambapo pembeni kuna maji na matope ambayo yamechanganyikana na vinyesi kutoka katika chemba za vyoo mbalimbali katika makazi ya watu.
Hii ndio hali halisi ya Chemba hii ambayo ipo ndani ya Hospitali ya Sinza Palestina.
Hizi ni chemba zaidi ambazo zipo nje na pia zimeungana na zilizopo ndani ya Hospital hiyo
Wagonjwa zaidi wakingojea waganga kufika pia kumalizia kusafishwa kwa vyumba hivyo ili wapate hudumiwa
Moja ya Chumba ambacho kilikuwa kimejaa tope kikingojea kusafishwa
Hapa hata hapapitiki
Baadhi ya viti vikiwa vimeegeshwa kwa ajili ya kungoja kufanya usafi
Hakuna mtu katika maeneo haya kutokana na mvua kubwa iliyonyesha
Kila kitu kimekaa hovyo hovyo baada ya mvua kubwa hiyo kunyesha
Baadhi ya vifaa vya kutibia wagonjwa vikiwa juu ya moja ya kitanda cha kutibia wagonjwa huku watu wakingoja huduma ya matibabu.
Huu ndio Mtaro wa maji machafu ambapo maji kutoka nje yamepita ndani ya hospitali hiyo na kusababisha maafa baada ya Mtaro huo kuziba. Picha zote na Dar es salaam yetu
No comments:
Post a Comment