Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMUAPISHA KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII LEO



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kaimu Rais Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimuapisha Dkt. Adelhelm James Meru kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii kwenye hafla fupi iliyofanyika leo Novemba 17,2014 Ikulu Dar es salaam.

Dkt. Adelhelm Meru (kulia) akiweka saini katika Kitabu mara baada ya kuapishwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Gharib (kushoto) akiweka saini katika kitabu mara baada ya kumuapisha Dkt. Adelhelm Meru kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Gharib (kushoto) akimkabidhi kitabu Dkt. Adelhelm Meru mara baada ya kumuapisha kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais na Kaimu Rais Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na utalii Dkt. Adelhelma James Meru wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuapishwa leo Novemba 17, 2014 Ikulu Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Gharib (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Dkt. Adelhelm Meru mara baada ya kuapishwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii leo Ikulu jijini Dar es Salaam.


Makamu wa Rais na Kaimu Rais Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na utalii Dkt. Adelhelma James Meru wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii mara baada ya kuapishwa leo Novemba 17, 2014 Ikulu Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.