Habari za Punde

*WADAU WA FILAMU WAKUTANA NA KUJADILI MAENDELEO YA TASNIA YA FILAMU NCHINI.


Katibu Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo (kulia) akieleza jambo wakati wa mkutano wa kujadili mambo yanayohusu tasnia ya filamu Tanzania uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa wa Bodi hiyo, Bw. Benson Mkenda.
Kaimu Mwenyekiti Bodi ya Filamu Tanzania, Sylivester Sengerema akieleza jambo wakati wa mkutano wa kujadili mambo yanayohusu tasnia ya filamu Tanzania uliofanyika katika ofisi za bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam. KWA PICHA ZAIDI BOFYA READ MORE
Kaimu Mwenyekiti Bodi ya Filamu Tanzania, Sylivester Sengerema (kushoto) akieleza jambo wakati wa mkutano wa kujadili mambo yanayohusu tasnia ya filamu Tanzania uliofanyika katika ofisi za bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mjumbe wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Bw. John Lister.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Bw. Simon Mwakifwamba akichangia mada katika mkutano uliohusu masuala ya tasnia ya filamu Tanzania uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Bw. Deosonga Njelekela.
Katibu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Bishop Hiluka akichangia mada katika mkutano uliohusu masuala ya tasnia ya filamu Tanzania uliofanyika katika ofisi za bodi ya Filamu Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Wadau kutoka Bodi ya Filamu Tanzania pamoja na Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) wakimsikiliza Katibu wa TAFF (hayupo pichani) wakati alipokuwa akichangia mada kuhusu masuala ya filamu nchini wakati wa mkutano uliofanyika katika Ofisi za Bodi ya Filamu jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO-DSM

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.