Habari za Punde

*BREAKING NEEEEWZZZ!!!!! MAGUFULI ATANGAZWA KUWA RAIS WA JAMHURI YA TANZANIA


TUME ya taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) imemtangaza Dkt. John Pombe Magufuli,  Mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM kuwa Mshindi wa nafasi ya Urais kwa baada ya kuibuka na jumla ya kura 8,082,935 sawa na 58.46% na kumbwaga mpinzani wake, Edward Ngoyai Lowassa, aliyekuwa akigombea nafasi hiyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) chini ya mwamvuli wa UKAWA ambaye aliyepata kura 6,072,848 sawa na 39.97%. 

 Kura za wagombea wengine ni:-
Anna Elisha Mgwira (ACT Wazalendo) kura 98,763 sawa na 0.65%
Chief Lutalosa Yemba (ADC) kura 66,049 sawa na 0.43%
Hashim Rungwe Spunda (Chauma) kura 49,256 sawa na 0.32%
Kasambala Janken Malik (NRA) kura 8,028 sawa na 0.05%
Lymo Macmillan Elifatio (TLP)8,158 sawa na 0.05%
Dovutwa Fahim Nasoro (UPDP) kura 7,785 sawa na 0.05%

Akitangaza Matokeo hayo, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva.

Dondoo muhimu:
Wapiga kura walioandikishwa walikuwa 23,161,440.
Waliojitokeza kupiga kura ni 15,589,636 sawa na 67.31%
Kura halali zilizopigwa ni 15,193,862 sawa na 97.46%
Kura zilizokataliwa ni 402,248 sawa na 2.58%.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.