Mkurugenzi Mkuu wa Fast Jet, Jimmy Kibati, akizungumza na waandishi wa habari leo mchana kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, wakati walipokuwa wakijitambulisha kuhusu udhamini wao kwa timu ya Taifa inayojiandaa kuelekea Algeria Novemba 16,ambayo Shirika hilo limetangaza kuidhamini Taifa Stars kwa kutoa ndege itakayobeba jumla ya watu 154. Kulia ni Katibu wa Kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda na (kushoto) ni Mkuu wa Masoko wa Fast Jet, Jay Petrie.
Katibu wa Kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda, akizungumza (kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa Fast Jet, Jimmy Kibati.
Afisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto, akizunguma.
Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo.
***********************************
Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar
Timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, inatarajiwa kusafiri na ndege ya binafsi ya kukodi ya shirika la Fastjet kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaochezwa Novemba 17 mjini Algiers.
Meneja Mkuu wa Shirika la Ndege la Fasjet kwa ukanda wa Afrika Mashariki, Jimmy Kibati amesema kampuni yao imefikia makubaliano na TFF ya kuwa msafirishaji rasmi wa timu ya Taifa kwa ajili ya mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi 2018 dhidi ya Algeria.
Jimmy amesema katika safari hiyo, Fastjet itatoa ndege yenye uwezo wa kubeba abiria 156 walioketi, sambamba na wafanyakazi wa ndenge, ambapo wao wametoa punguzo la asilimia 35 katika gharama nzima ya safari ya kuelekea Algeria.
Aidha Jimmy ameongeza kuwa safari hiyo itakua ni ya masaa 7 ambapo ndege ikitoka Dar es salaam itatua Djamena – Chad kuongeza mafuta kabla ya kuendelea tena na safari mpaka nchini Algeria.
Naye katibu wa kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda aliwashukuru Fastjet kwa kukubali kuwa wasafirishaji rasmi wa TaifA Stars kwa mechi dhidi ya Algeria, huku akisema gharama za safari za mtu mmoja kusafiri ni dolla 800 kwenda na kurudi.
Teddy amewaomba watanzania, wapenzi, washabiki wa mpira wa miguu wanaotaka kusafiri kufika ofisi za TFF zilizopo Karume kwa ajili ya kujiandiksha na kuelekea taratibu nzima za safari.




No comments:
Post a Comment