Kocha wa Chelsea, Jose Mourihno, akibaki mdomo wazi baada ya kuchapwa bao 3-1 na Liverpool katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wao wa nyumbani jana ikiwa ni mechi ya kwanza kati ya mechi mbili alizopewa kubadili matokeo na kuirudisha timu hiyokwenye mstari kabla ya kufungashiwa virago.
Kocha huyo kwa hivi sasa anazidi kukalia kuti kavu kutokana na timu yake kuzidi kuboronga katika Ligi hiyo ya England kwa kupoteza michezo kibao, ambapo inaelezakuwa huenda ikawa ni hujuma ya wachezaji wake wanaomhujumu ili aondoshe kikosini kutokana na matukio kadhaa yaliyotokea siku za nyuma ikiwa ni pamoja na lile lililoitwa la udharilishaji dhidi ya aliyekuwa Daktari wa timu hiyo mwanamama.
Kwamatokeo hayo sasa, Mourinho amebaki na mechi moja mkononi itakayoamua mustakabali wa yeye kubaki kukiongoza kikosi hicho ama la kulingana na matokeo ya mechi hiyo ijayo.
Ila kwa habari zilizoripotiwa na mtandao wa Sky News, zinasema kuwa tayari Club ya Chelsea imeshathibitisha kuachana na kocha huyo.
Ila kwa habari zilizoripotiwa na mtandao wa Sky News, zinasema kuwa tayari Club ya Chelsea imeshathibitisha kuachana na kocha huyo.






Bao la tatu lilifungwa na Christian Benteke aliyeingia kipindi cha pili na kuifungia timu yake bao la tatu na kufanya matokeo kuwa 3-1 dhidi ya wenyeji Chelsea waliokuwa nyumbani kwenye Uwanja wao Stamford Bridge.
No comments:
Post a Comment