Gari ndogi lenye namba za usajiri Z 511 FG, likiwa limepata ajali maeneo ya Kijiji cha Kibele Wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja leo majira ya saa nane mchana, ambalo lilikuwa likiendeshwa na Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja.
Aidha imeelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi ambapo dereva wa gari hilo dogo aona ya Spacio alishindwa kulimudu gari hilo na hatimaye kuacha barabara na kugonga mnazi ambao uliangukia gari hilo na gari kuwaka moto.
Hata hivyo Dereva huyo aliokolewa na wasamaria wema ambapo alikuwa amebanwa na air bags zilizofyatuka na kuokoa uhai wake. Alipata majeraha madogo ya kuchubuka kwenye mikono yake iliyokuwa inavuja damu.
Ajali mbaya
No comments:
Post a Comment