Meneja Masoko wa Kinywaji cha John Worker na Mkuu wa Kitengo uboreshaji, Stanley Samtu (wapili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa mwanamuziki kutoka nchini Uingereza, Arjuni Coomeraswamy (wa pili kulia) aliyewasili nchini jana kwa ajili ya kupiga shoo kadhaa, ambapo anaanza na shoo ya kesho mjini Zanzibar. Mwanamuzki huyo amedhaminiwa na Kinywaji hicho cha John Worker. Half fupi ya utambulisho huo ilifanyika jana jioni kwenye Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam, Kulia ni Miss Tanzania 2007, Richa Adhia na (wapili kulia) ni Mwanamuziki Linah Sanga, atakayemsindikiza mwanamuziki huyo katika shoo kadhaa.
Miss Tanzania 2007, Richa Adhia akizungumza katika mkutano huo.
Mwanamziki wa Uingereza, Arjun Coomeraswamy akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)juu ya ujio wake ambapo pia anatarajia kukutana na watu mbalimbali katika Ukumbi wa Viva Tower jijini Dar es Salaam na Jumamosi atafanya shoo Zanzibar katika ukumbi wa Kendwa Rocks Beach Resort.
Msanii Linah Sanga akiongea machache.
No comments:
Post a Comment