Habari za Punde

*KAZI IMEANZA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSTUKIZA WIZARA YA FEDHA LEO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.  Servacius Likwelile alipotembelea ofisi za Wizara ya Fedha.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipata ufafanuzi kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.  Servacius Likwelile wakati wa ziara hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na uongozi wa Wizara ya Fedha.
**********************************
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amefany aziara ya kushtukiza katika Ofisi za Wizara ya Fedha leo Ijumaa tarehe 6 Novemba, 2015.

Katika ziara hiyo Mhe.Rais alipata fursa ya kutembelea baadhi ya Ofisi za Wizara na baadae kuzungumza na Viongozi wa Wizara ili kufahamu changamoto ambazo zinaikabili Wizara ya Fedha.

Wakati akimkaribisha Mhe.Rais Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile alimueleza kuwa Wizara ya Fedha inakabiliwa na changamoto kubwa inayotokana na makusanyo ya mapato ya ndani.

  Miongoni mwa sababu ni misamaha ya kodi, wafanyabiashara wengi hasa wakubwa kukwe pakodi, makusanyo yasiyoridhisha ya maduhuli na kutokulipwa kwa kodi za majengo.Aidha Dkt. Likwelile alishauri ni bora kuwekwa mifumo mizuri, ikiwemo matumizi ya Tehamana EFDs.
“Pamoja na ziara yangu kuwa ni ya kustukiza nimefurahi sana kukuta Viongozi wote wapo ofisini  na wanafanyakazi. Jambo hili limenipa faraja kubwa. Ziara yangu  
ya kuja hapa nimejifunza na kujua changamoto zipi zinazowakabili”. Alisema Mhe. Rais.
Nimesikia changomoto nyingi naninaagiza kuwa muhakikishe walipakodi wakubwa wanalipa kodi na kusimamia kikamilifu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili iweze kukusanya kodi kikamilifu na  sikuwabana wafanyabiashara wadogo wadogo.
Mhe.Rais aliwataka Viongozi wa Wizara kufanya kazi kwa bidii ili kuvuka lengo.

Imetolewana;
MsemajiwaWizarayaFedha
IngiahediC.Mduma

6.11.2015

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.