Barabara mpya ya Morogoro jinsi ilivyoharibika eneo la Fire na kusababisha eneo hilo kufungwa na magari kuruhusiwa kupita kwenye barabara ya mabasi yaendayo kasi kwa muda, lakini toka ilipochimbuliwa kwa ajili ya matengenezo hadi sasa ni zaidi ya mwezi matengenezo hayajakamilika jambo ambalo linasababisha usumbufu kwa watumiaji wa njia hiyo na msongamano mkubwa wa magari hasa nyakati za asubuhi na jioni.
Kabla ya kuchimbuliwa kama hivi eneo hili lilikaa zaidi ya mwezi likiwa linatiririsha maji yaliyokuwa yakitoka ardhini huku yakichimba eneo hilo na magari yakipita kwa taabu kwa kusubiriana ili kukwepa mashimo hayo.
Hivi sasa eneo hili ndilo limekuwa kituo cha daladala cha dharura jambo linalosababisha foleni....
Baadhi ya abiria wakisubiri usafiri katika eneo hilo....
No comments:
Post a Comment