Habari za Punde

*WATOTO WA MITAANI WAONYESHANA UMWAMBA NA UMAHIRI WA KUPIGANA VITA YA MAWE

 Vijana ambao hawakuweza kufahamika majina yao mara moja, wanaohisiwa kuwa ni watoto wa mitaani (chokoraa) wanaoishi na kufanya shughuli zao pembezoni mwa barabara ya Ali Hassan Mwinyi eneo la Morocco, wakitwangana kwa mawe wakati walipkuwa wakipigana huku waliowengi wakimchangia kijana huyu mmoja (kushoto) ambapo aliwasambaratisha kwa mawe hawa wote wanaoonekana (kulia).  Haikuweza kufahamika chanzo cha ugomvi wao. Vita hii iliwafanya madereva waliokuwa wakipita eneo hilo kuogopa kukatiza na kusimama mbali ili kupisha vurugu hiyo na vita ya mawe iliyokuwa ikirindima, kwa kuogopa kuvunjiwa vioo.
 Jiwe likitua kichwani huku jingine likiwa hewani.... na akIjaribu kukwepa...
 Baada ya kukwepa jiwe la pili akaamua kutoka nduki huku mwingine akijiandaa kurusha kumsaidia mwenzake... na wengine wakikimbilia vichakani.
Dogo akitoka nduki kuokoa maisha yake  na sura yake isiharibiwe kwa mawe yaliyokuwa yakirindima mfano wa risasi mfululizo...

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.