Habari za Punde

*ENG. STELLA MANYANYA KUWATIMUA KAZI WALIMU WAKUU

Naibu Waziri wa Elimu, Ufundi, Sayansi na Teknolojia, Eng. Stella Manyanya, Mwenyekiti wa Tatola kwa nchi za Afrika na Arabuni, Jean Christian Bergeron, kwa pamoja wakikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa hafla ya makabidhiano ya madawati 1000, yaliyotolewa na kampuni ya mafuta ya Total, kwa shule 10 za Dar es Salaam na Bagamoyo.

Weingine ni Mkurugenzi Mkuu wa Total Tanzania, Tarik Moufaddal , Mwenyekiti wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Prof. Naomi Katunzi, na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, TEA, Joel Laurent. Photo by PPR
*****************************************************
By Pascal Mayalla                
Katika kuendena na kasi ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Naibu Waziri wa Elimu, Ufundi, Sayansi na Technolojia, Eng. Stella Manyanya, afanya ziara ya kushtukiza Mamlaka ya Elimu, TEA, akuta mambo safi!,  Atishia Kutimua Kazi Walimu Wakuu wote, ambao wanafunzi wao, wataingia darasa la tatu bila kujua kusoma na Kuandika.

Naibu Waziri Manyanya, aliyasema hayo, wakati wa ziara ya kushtukiza aliyoifanya kutembelea Mamlaka ya Elimu Tanzania, TEA ambapo alikuta mambo safi.

Kuhusu timua timua ya waalimu wakuu wa shule za Msingi za Umma, Eng. Manyanya amesema, emeshuhudia wanafunzi wa shule za awali, yaani chekechea, ambao wanajua kusoma na kuandika, hivyo haiwezekani, mwanafunzi wa darasa la tatu shule za umma, asijue kusoma na kuandika!, huu utakuwa ni uzembe wa waalimu.

 Hivyo, watafanya ukaguzi kwa shule zote za umma, na wakikuta kuna wanafunzi wa darasa la tatu hawajui kusoma na kuandika!, ni bora waalimu wakuu wa shule hizo, waandike baua za kuachia ngazi kwa kushindwa kazi, kabla hawafikiwa, maana wakifikiwa , watafukuzwa kazi!.

Ziara hiyo ilifutiwa na tukio la kukabidhiwa madawati 1000, na kampuni ya mafuta ya Total, iliyokwenda sambamba na ufunguzi wa kituo kipya cha mafuta cha Ukuni, kilichopo wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.  

Akikabidhi madawati hayo, Mwenyekiti wa Total kwa Bara la Afika, na Arabuni, Jean –Christian Begeron  aliahidi Total kuendelea kuchangia mipango mbalimbali ya kijamii na kueleza kuwa kampuni ya Totali, sio tuu ipo kwa ajili ya kufanya biashara, bali ni sehemu ya Jamii, hivyo inaguswa na matatizo ya jamii husika, na kuchangia katika utatuzi wa matatizo ya kijamii kama wajibu na sio hisani.

Uzinduzi wa kituo hicho ni  katika juhudi za Kampuni ya Total kupanua wigo wake wa kibiashara, kuwafikia wateja wengi zaidi, na kutoa huduma bora n aza kisasa zaidi,   ndio maana Total Tanzania,   imezindua kituo kipya cha Mafuta, chenye muonekano mpya , kwa ajili ya kuuizia bidhaa za Total, na  huduma  za kisasa,  kiitwacho Ukuni Service Station, kilichopo  Barabara ya Msata , Wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.

Uzinduzi wa kituo hicho kipya, umekwenda sambamba na utoaji wa madawati 1000 kwa shule  9 za Dar es Salaam na moja ya Bagamoyo.  ambapo zoezi hili la utoaji wa madawati, limefanikishwa kwa kampuni ya Total Tanzania ikishirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) pamoja na Kampuni ya Katson LTD,
 
Total Tanzania, inawashukuru wateja wake wa m i koa y a Dar esalaam na Bagamoyo kwa kutoa madawati kwa shule 9 za Dar es Salaam na shule moja Bagamoyo. Kila shule itapata madawati 100 na kufanya idadi ya madawati 1000. Total imekuwa ikitoa madawati kuanzia  mwaka 2013 mpaka  mwaka huu 2015 Total ime kwisha toa  jumla ya madawati 3000 katika shule za msingi , yenye thamani ya  zaidi shilingi milioni 300.

Mkurugenzi wa Total Tanzania, Bwana Tarik Moufaddal  amesema  Total Tanzania, ,itaendelea kutoa ushirikiano na serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Mhe. Dr. John Pombe Magufuli, katika miradi mbalimbali ya kijamii ili kuisaidia  serikali yetu kuboresha hali ya elimu nchini” . Bwana  Moufaddal alizitaja shule zinazopokea madawati kuwa ni BUYUNI II, MJIMPYA, PUGU KAJIUNGENI, NZASA, SANDALI, KIZINGA, MTONI NIANJEMA, MAGOMENI, MSHIKAMANO.  
 
Akipokea msaada huo, Naibu waziri wa Elimu, Eng. Stella Manyanya “ Aliishukuru kampuni ya Total Tanzania, kwa misaada yake na  kuyahimiza  makampuni megine ya umma na binafsi kuiga mfano wa Total Tanzania na kuipa jukumu la ziada TEA kuhakikisha inafanya kampeni maalum ya uhamasishaji ili mashiika, makapuni na watu binafsi wachangie ili madawati  ya kutosha yapatikane, hakuna tena mwanafunzi kukaa chini!.

Total Tanzania kampuni ambayo imekuwa nchini kwa miaka 46, inajikita katika kutoa huduma bora na za uhakika kwa wateja wake. Inawahakikishia wateja wake bidhaa zilizo na viwango vya hali ya juu kuanzia Mafuta ya gari, Vilainishi, Taa za sola za Awango, Kadi za mafuta za Total na huduma zingine zinazopatikana vituoni kama kuosha magari na duka. Kampuni inalenga kufanya vituo vyake ni sehemu ambayo mteja wake anapata huduma zote muhimu ikiwa utengenezaji wa magari, chakula  na bidhaa za nyumbani kwenye maduka yake.
 Naibu Waziri wa Elimu, Ufundi, Sayansi na Teknolojia, Eng. Stella Manyanya, akipongezana na Mwenyekiti wa Tatola kwa nchi za Afrika na Arabuni, Jean Christian Bergeron baada ya makabidhiano. 
 Naibu Waziri wa Elimu, Ufundi, Sayansi na Teknolojia, Eng. Stella Manyanya, a(kushoto) akiketi Mwenyekiti wa Tatola kwa nchi za Afrika na Arabuni, Jean Christian Bergeron na Mkurugenzi Mkuu wa Total Tanzania,Talik Moufaddal, katika madawati ikiwa kama ishara ya kupokea jumla hya madawati 1000, kutoka kwa kampuni ya mafuta ya Total, yaliyotolewa kwa ajili ya shule 10 za Dar es Salaam na Bagamoyo.

Picha na pamoja ya viongozi pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hizo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.