Na Skolastika Tweneshe MAELEZO
Wafanyabiashara wameaswa kutoendelea na uuzaji wa vyakula na matunda yaliyomenywa katika maeneo yaliyo wazi na yoyote atakayeendelea kuuza atachukuliwa hatua kali za kisheria hii ni kutokana na kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Msemaji wa Manispaa ya Ilala Bw. David Langa alipozungumza na mwandishi kuhusu tamko la Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu kupiga marufuku uuzwaji wa vyakula au matunda yaliyomenywa katika maeneo ya wazi.
“Kwa mfanyabiashara yoyote tutakayemkamata tutamfikisha mahakamani na adhabu yake ni faini ya sh 30,000 au kwenda jela miezi mitatu au vyote kwa pamoja.” alisema Langa.
Aidha Bw. David Langa amesema katika ukutekelezaji wa suala hili watendaji wa kata wanahusika moja kwa moja kusimamia na kufuatilia kwa karibu operesheni hii, na kusisitiza sheria za Afya kuzingatiwa na kutokuwa na huruma kwa yeyote atakayevunja sheria.
Kumekuwa na uuzwaji wa vyakula na matunda yaliyomenywa jijini Dar es salaam hasa maeneo ya katikati ya jiji hivyo kuhatarisha afya za wananchi, ila Serikali kupitia halmashauri zake imeahidi kulitilia mkazo suala hili.
No comments:
Post a Comment