Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwasili
kituo cha tiba za asili na mbadala cha Kliniki ya Foreplan Herbal cha Dkt. Juma
Mwaka leo jioni alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho kilichopo
eneo la Ilala Bungoni jijini Dar es salaam kujionea namna kituo hicho
kinavyotoa huduma za kiafya.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi Kigwangalla akiongea na
Husna Maokola Majogo (aliyekaa) mara baada ya kuwasili kituo cha tiba za asili
na mbadala cha Kliniki ya Foreplan Herbal cha Dkt. Juma Mwaka leo jioni
alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho kilichopo eneo la Ilala
Bungoni jijini Dar es salaam kujionea namna kituo hicho kinavyotoa huduma za
kiafya.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia
baadhi ya vifaa vinavyotumika kutibia wagonjwa katika kituo cha tiba za asili
na mbadala cha Kliniki ya Foreplan Herbal cha Dkt. Juma Mwaka leo jioni
alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho kilichopo eneo la Ilala
Bungoni jijini Dar es salaam kujionea namna kituo hicho kinavyotoa huduma za
kiafya. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,wizara hiyo
Nsachris Mwamwaja.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia baadhi dawa zinavyotumika kutibia wagonjwa katika kituo cha tiba za asili na mbadala cha Kliniki ya Foreplan Herbal cha Dkt. Juma Mwaka leo jioni alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho kilichopo eneo la Ilala Bungoni jijini Dar es salaam kujionea namna kituo hicho kinavyotoa huduma za kiafya.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi Kigwangalla akiongea na
baadi ya watoa huduma (waliovaa sare nyeusi) wakati wa ziara ya kushtukiza
katika kituo cha tiba za asili na mbadala cha Kliniki ya Foreplan Herbal cha
Dkt. Juma Mwaka kilichopo eneo la Ilala Bungoni jijini Dar es salaam. Wa kwanza
kushoto ni Afisa Habari Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,wizara hiyo Catherine
Sungura.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi Kigwangalla akipita kuangalia maeneo ya kutolea huduma katika kituo cha tiba za asili na mbadala cha Kliniki ya Foreplan Herbal cha Dkt. Juma Mwaka leo jioni alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho kilichopo eneo la Ilala Bungoni jijini Dar es salaam kujionea namna kituo hicho kinavyotoa huduma za kiafya. Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO
*****************************************
Na Eleuteri Mangi
-MAELEZO
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa siku
saba kuchunguza kituo cha tiba za asili na mbadala cha Kliniki ya Foreplan
Herbal kinachomilikiwa na Dkt. Juma Mwaka.
Dkt. Kigwangalla ametoa
agizo hilo kufuatia ziara ya kushtukiza aliyoifanya katika kituo hicho kilichopo
eneo la Ilala Bungoni jijini Dar es salaam kujionea namna kituo hicho
kinavyotoa huduma za kiafya.
Dkt. Kigwangalla alifikia
hatua hiyo ya uchunguzi baada ya mazingira ya mapokezi ya msafara wake kutopewa
ushirikiano wakati wa ziara hiyo ambapo kulizua hali ya wasiwasi kwa watoa
huduma wa kituoni hapo na ndipo alipomuagiza Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Tiba
Asilia na tiba Mbadala Dkt. Mhame Paulo kufanya uchunguzi kupitia Baraza la
Tiba Asilia kama kituo hicho kipo kisheria.
Katika hali
isiyotarajiwa, viongozi na watoa huduma wa kituo hicho walipogundua kuna ugeni
wa Naibu Waziri huyo waliacha ofisi zao na kutoweka kituoni hapo na hata
waliokuwepo hawakuwa tayari kuzungumzia hali ya matibabu kituoni hapo.
“Mkurugenzi wa kituo
hiki tunafahamu na alikuwepo hapa, amepanda gari dakika 10 kabla hatujaja hapa,
Matabibu, wafamasia na watu wa vipimo wametoroshwa kupitia mlango wa nyuma
tusionane nao kuona namna wanavyotoa huduma”,
“Sasa tambueni kuwa
Serikali ipo na inafanya kazi yake, nitakuja tena wakati wowote ninaoujua mimi”
alisisitiza Dkt. Kigwangalla.
Dkt. Kigwangalla
amelitaka Baraza la Tiba Asilia kufanya uchunguzi ndani ya wiki moja kuibaini taaluma
za watoa huduma kituoni hapo, aina ya miti shamba inayotumika kama dawa ili
kujua kama Watanzania wanapata huduma halali na kama siyo halali Serikali
ichukue hatua satahiki dhidi yao.
Aidha, Dkt. Kigwangalla
ambaye pia ni Mtaaluma katika masuala ya afya kutoka Chuo Kikuu Cha Sayansi Na
Tiba Muhimbili na Chuo Cha Karolinska cha nchini Sweden alisema Mkurugenzi wa
kituo hicho amekosa weledi na anajiita “Dkt” Juma Mwaka, na kusisitiza kuwa miongoni
mwa makosa ya kimaadili ya kidaktari wa kisasa na kujitangaza kupitia vyombo
vya habari kitu ambacho ni kinyume na miiko ya taaluma hiyo.
Katika hatua nyingine, Dkt.
Kigwangalla amemuagiza Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asilia na Tiba Mbadala
Dkt. Mhame Paulo kwa kushirikiana na Baraza la Tiba Asilia wafanye pia uchunguzi
kwa Dkt. Rahabu Rubago anayetibu vidonda vya tumbo pamoja na
Dkt Isack Ndodi anayetibu magonjwa mbalimbali kwa kutumia tiba mbadala na
kupeleka taarifa hiyo ofisini kwa Naibu Waziri huyo ndani ya siku saba.
Kwa upande wake mmoja
wa watoa huduma kituoni hapo Teddy Mbuya alisema kuwa yeye siyo msemaji,
viongozi hawakuwepo ambapo alimuongoza Naibu Waziri maeneo mbalimbali kujionea
hali ilivyo kwenye vyumba vya kutolea huduma za vipimo, mapokezi, duka la dawa
asilia na sehemu ya kupumzika wagonjwa wakiwa wanasubiri kuhumiwa.





No comments:
Post a Comment