Jacquiline
Mrisho
RAIS wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema Serikali ya
Tanzania inatekeleza mikakati ya kuweka mazingira bora ili sekta isiyo rasmi iweze
kuchangia vizuri katika maendeleo ya Taifa.
Mhe. Magufuli aliyasema
hayo wakati akifungua Maonesho ya Wajasiriamali ya Juakali/Nguvu Kazi kwenye viwanja
vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Akifungua kwa
niaba ya Rais, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Said Meck Sadiki
alitaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuweka mpango maalumu wa kurasimisha
shughuli za Sekta isiyo rasmi (MKURABITA).
Alisema mpango
hu unatoa fursa ya mikopo nafuu kuwawezesha wajasiriamali na kuwapa elimuya
namna bora ya kufungasha bidhaa zinazozalishwa.
Mkuu wa mkoa wa
Dar es Salaam Mheshimiwa Said Meck Sadiki maonesho hayo yameshirikisha
wajasiriamali zaidi ya 700 kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Pia maonesho
hayo wamehudhuriwa na Mabalozi kutoka nchi wanachama, Makatibu
Wakuu,Wakurugenzi, Wenyeviti wa Wajasiriamali hao kutoka Nchi wanachama.
Maonesho hayo
pia yameshirikisha Taasisi mbalimbali zikiwemo Taasisi za Fedha,Taasisi ya
Mifuko ya Jamii na Mamlaka ya usajili (BRELA).
Kabla ya
kufungua maonesho hayo, Mheshimiwa Said Meck
Sadiki alitembelea baadhi ya
mabanda ili kuona kazi za wajasiriamali hao.
Mwenyekiti wa
Shirikisho la Wajasiriamali Wasiorasimishwa Afrika Mashariki, Josephat
Rweyemamu alisema madhumuni ya maonesho hayo ikiwemo kuwawezesha wajasiriamali
kupanua masoko ya bidhaa zao pamoja na changamoto wanazozipata wajasiriamali
hao.
Alieleza baadhi
ya changamoto kuwa ni ukubwa wa kodi, pia aliiomba Serikali kufungua kiwanda
cha Urafiki ili kuwasaidia wajasiriamali
pia kuwatengea maeneo maalum kwa ajili ya kufanyia biashara zao.
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt Joyce Mapunjo alieleza
kufurahishwa na bidhaa za wajasiriamali.
“Nimefurahishwa
sana na bidhaa mbalimbali toka kwa wajasiriamali wa Afrika
Mashariki na Serikali zetu za Afrika Mashariki zinatambua mchango wa Sekta
isiyo rasmi na ndio mana tukawa na maonesho haya”.alisema Mhe. Dkt. Mapunjo.
Hata hivyo,
alisema pamoja na mafanikio hayo, Serikali za nchi wanachama zinatambua kwamba
Sekta isiyo rasmi inakabiliwa na vikwazo na changamoto nyingi ambazo zinadumaza
maendeleo ya Sekta hii isiweze kukuwa na kuwa Sekta rasmi.
Rais John Pombe
Magufuli amewahakikishia wajasiriamali wa Tanzania kuwa wameshayajadili na
kwasasa wanayafanyia kazi.
“Kuna hatua
ambayo Serikali ya Tanzania inatekeleza katika kuweka mazingira bora ili Sekta
isiyo rasmi iweze kuchangia vizuri katika maendeleo ya Taifa letu” aliongeza.
Maonesho hayo yalianzishwa tangu mwaka 1999 na
hufanyika katika Nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki kwa mzunguko.
Kwa Tanzania
haya ni maonesho ya Tano kufanyika na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Nunua bidhaa
zilizozalishwa na Afrika Mashariki ili kukuza uchumi wa Afrika Mashariki”.

No comments:
Post a Comment