Afisa Uvuvi
kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na
Uvuvi Bw. Silas William akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu hatua
zinazochukuliwa na Serikali katika kuwainua wavuvi wadogo hapa nchini ili
kushiriki katika kukuza uchumi wa Taifa. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na
Uvuvi Bi Fatma Sobo.mwisho kushoto ni Mkuu wa
kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na
uvuvi Bi Judith Mhina.
Waandishi wa
habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mkutano kati yao na
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ambao pamoja na mambo mengine
ulibainisha kuwa Serikali imejipanga kukomesha uvuvi haramu hapa nchini hasa
kwa kutumia mabomu kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais,Wizara ya Mali asili na
Utalii, Wizara ya Nishati na Madini,Wizara ya mambo ya Ndani na ile ya Katiba
na Sheria. Picha na
Frank Mvungi-Maelezo
No comments:
Post a Comment