Habari za Punde

*RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI WAPYA IKULU DAR

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais John Pombe Joseph Magufuli (katikati) akimuapisha Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashantu Kijaji leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashantu Kijaji (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kaitibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) mara baada ya hafla ya kuapishwa Mawaziri na Manaibu Waziri wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais John Pombe Joseph Magufuli. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara Utawala Wizara ya Fedha na Mipango Deodata Makani.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meky Sadik walipokutana kwenye hafla ya kuapishwa Mawaziri na Manaibu Mawaziri Ikulu Dar es salaam leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kumpongeza  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Utumishi na Utawala Bora  Mhe.  George Simbachawene  baada ya  hafla ya kuapishwa Mawaziri na Manaibu Mawaziri Ikulu Dar es salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Januari Yussuf Makamba akipitia mafaili alipowasili Ofisini kwake mtaa wa Luthuli Dar es salaam muda mfupi baada ya kuapishwa na Rais Mhe. John Pombe Magufuli Ikulu Dar es salaam

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga J Mpina akipitia mafaili alipowasili Ofisini kwake mtaa wa Luthuli Dar es salaam muda mfupi baada ya kuapishwa Ikulu Dar es salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli katikati, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan Kulia na Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim kushoto, wakiwa katika mpicha ya pamoja na Mawaziri na Manaibu Mawaziri mara baada ya kuapishwa Mawaziri hao

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.