Mkurugenzi wa Tume ya Haki za Binadamu Bw. Francis Nzuki akiongea na waandishi wa habari katika kongamano la kujadili malengo endelevu kufikia malengo ya Milenia jijini Dar es salaam leo.
Wadau kutoka sehemu mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja waliposhiriki kongamano la kujadili malengo endelevu kufikia malengo ya Milenia jijini Dar es salaam leo.
Mwakilishi kutoka Shirika linalohudumia Wazee (HELPAGE) na pia ni mshiriki Bw. Joseph Mbasha
akiongea na waandishi wa habari katika kongamano la kujadili malengo endelevu kufikia malengo ya Milenia jijini Dar es salaam leo.
Baadhi ya wadau kutoka sehemu mbalimbali wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokua ikitolewa na mgeni rasmi hayupo pichani wakati wa kongamano la kujadili malengo endelevu kufikia malengo ya Milenia jijini Dar es salaam leo.
**********************************************
Na Shamimu Nyaki-Maelezo, Dar es salaam
Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu duniani ambayo ni tarehe10 Disemba mwaka huu,Tume ya haki za binadamu na Utawala bora leo imeandaa kongamano la siku moja kujadili Mpango wa Maendeleo Endelevu unaotarajia kuanza rasmi januari mwaka2016.
Mgeni Rasmi katika kongamano hilo Bi Rehema Ntimizi kutoka Tume ya haki za binaadamu ameiomba jamii kushiriki kwa ukamilifu katika kuleta maendeleo yao wenyewe na taifa kwa ujumla kwa kuwa maendeleo yanaanza na watu wenyewe kwa kuhakikisha wanaondokana na umasikini, kuwa na afya bora ,pamoja na elimu na kutambua kuwa ni haki yao kuwa na uwelewa wa suala hilo.
“Binadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa hivyo wote tuwajibike katika maendeleo”Alisema bi Ntimizi.
Bi Rehema ameongeza kuwa dunia nzima kwa sasa inashirikisha makundi yote katika jamii katika kutoa maamuzi hasa yale yaliyosahaulika kama wanawake,wazee na watoto waishio vijijni hivyo wakati umefika sasa kwa kila mtu katika jamii kushiriki hatua zote za maendeleo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano la kujadili mpango huo leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Tume ya haki za Binaadamu bw Francis Nzuki ameeleza kuwa lengo la kongamano hilo ni kujadili mpango huo wa maendeleo endelevu jinsi gani utaleta matokeo chanya katika kufikia malengo ya millenia ifikapo mwaka 2030.
Ameongeza kuwa mpango huo umejikita katika malengo kumi na saba ambayo miongoni mwao ni kuondoa umaskini,kutoa Elimu bora, afya bora pamoja na maji safi kwa kila kundi lililopo katika jamii ambao ni vijana,wazee, wanawake, pamojana watoto katika jamii ya Watanzania ili kuweza kufikia malengo ya millenia.
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa Tume itaanzisha utaratibu wa kutembelea hospitali za umma kuanzia ngazi ya mkoa hadi kijiji ili kuweza kubaini
malalamiko na changamoto wanazopata wananchi ,lakini pia kutoa elimu jinsi watakavyoweza kusaidiwa na tume pale wanakutana na changamoto katika suala
linalohusu haki na utu wao.
Kauli mbiu katika kongamano hilo ni “Haki zetu uhuru wetu daima”. Aidha mshiriki kutoka shirika linalowahudumia wazee linaloitwa Helpage Intanational Fund Bw Joseph Mbasha amesema kuwa wazee wanapaswa kushirikishwa katika masuala yote ya maendeleo kwa kuwa nao ni binaadamu na wana uhuru wa kutoa mawazo na kupewa afya bora, kuondokana na umaskini lakini pia kumiliki ardhi.
“Kila mmoja ashiriki katika maendeleo yake na Taifa kwa ujumla”Alieleza
Mbasha.
Kongamano hilo limehudhuriwa na wadau mbalimbali wa haki za binaadamu wakiwemo Haki Elimu,YUNA,Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Chuo kikuu cha Dar es salaam pamoja na Chuo cha Uhasibu.
No comments:
Post a Comment