Habari za Punde

*TUTASIMAMIA KAZI ZA WASANII KWA NGUVU ZOTE-NAPE

  Waziri wa Habari, Utamaduni,S anaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na wadau mbalimbali kutoka BASATA,COSOTA,BODI YA FILAMU,CMEA NA WASANII hiijijini Dar es Salaam, leo juu ya kuendelea kusimamia haki ya wasanii na kuhakikisha kila msanii anapata anachostahili kupitia Sanaa yake na kwamba Serikali imeweka nguvu kubwa katika eneo hilo.
*********************************************************
 Na Daudi Manongi-WHUSM
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amehaidi kusimamia kazi za wasanii kwa nguvu zote na kuhakikisha haki ya kila mtu inapatikana.
Mhe Nape alisema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya vyombo vya habari (televisheni na Redio) kuanza kulipia mirahaba kwa wasanii wa muziki kuanzia tarehe mosi januari 2016.
“Serikali imeweka nguvu kubwa kwenye Sanaa,tutashirikisha wadau wote ili kusiwe na malalamiko katika jambo hili na tumeamua kulisimamia suala hili la Sanaa ili liwe suala la kiuchumi na litupa+e mapato pia kwani wasanii hawa watalipa kodi pia,COSOTA iweke wazi mapato haya na msimamie kazi zao vyema”Alisema Mhe .Nape

Mhe Nape ambae alikuwa pamoja na waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage katika mkutano huo alisema serikali ya awamu ya tano iko imara na imeamua kufanya kazi kwa karibu na wasanii kwani kwa muda mrefu kazi zao zimekuwa hazilipwi inavyotakiwa.

Naye Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage alisema wasanii wanitaji kwenda COSOTA kwa ajili ya kuwasilisha taarifa maalum za nyimbo zao ili zitambulike rasmi na kuanza kulipwa kwani kufikia tarehe mosi januari 2016 vyombo vya habari vitaanza kulipia mirahaba kwani sheria hiyo ipo tayari.

“Nimepata taarifa kuwa utara+bu huu ni mzuri kwani utakuwa pia na nafasi ya vituo kujadili na COSOTA wakati wa kupata leseni,pia taarifa za migao ya pesa hizo zitakuwa wazi na kwa waka+.Pia nimejulishwa kuwa COSOTA na CMEA (Copyright Management East Africa) wanendelea kutoa semina kwa wasanii na wanatarajia kufanya warsha na vituo vya Utangazaji na mikoani pia ili kutoa elimu ya utaratibu huu”Alisema Mhe.Mwijage.

Nae msanii wa kundi la Weusi Nikki wa Pili aliishukuru serikali kwa kuwa karibu na wasanii na pia aliomba Sera zibadilishwe na ziwe elekezi na pia kodi ipunguzwe kwenye vifaa vya muziki ili wasanii waweze kuviingiza nchini ili upigaji wa video na kurekodi uwe wa bei nzuri na wasanii hawa
wasiende nje ya nchi kurekodi kwani wanatoa pesa nyingi sana.

Tunaiomba Cosota ifanye kazi na CMEA (copyright Management of East Africa) ili wasanii wafaidike,na pia sera zibadilishwe na ielekezwe kuboresha teknolojia ili ubora wa muziki na video zetu ushindane na wa nchi zingine’’Alisema Nikki.

Kwa upande wake Meneja wa Operesheni wa Copyright Management East Africa (CMEA) ambao ndo watasimamia haki miliki za kazi za wasanii na itawawezesha wasanii na watayarishaji wa muziki
kufahamu takwimu sahihi za nyimbo zilizochezwa kwa siku,wiki,mwezi na mwaka na kulipwa mirahaba yao.

Mkutano ulihudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka wizara ya Viwanda,Biashara na uwekezaji bodi ya Filamu Tanzania,Cosota,basata na wawakilishi wa wasanii.
  Meneja wa Operesheni wa kampuni ya CMEA (Copyright Mnagement East Africa)ambao imetengeneza utaratibu wa kusimamia haki miliki za kazi za wasanii waukanda wa Afrika Mashariki akichangia jambo katika mkutano na waandishi wa habari juu ya wasanii kuanza kulipwa mirahaba kuanzia mwakani na wamiliki wa vyombo vya habari.
  Katibu mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi Joyce fisoo (kushoto) akiwa pamoja na afisa mtendajiwa COSOTA Bi. Doreen Sinare (katikati) na Paul Matthysse ambaye ni afisa mtendaji mkuu wa CMEA wakati wa mkutano na waandishi wa habari juu ya vyombo vya habari
  Mwanamuziki wa kundi la Weusi Nikki wa Pili akichangia hoja katika mkutano na waandishi wa habari juu ya wao kuanza kulipwa mirahaba kupitia kazi zao. Nikki wapili aliiomba serikali kupunguza kodi katika vifaa vya kurekodia filamu na muziki ili wasanii watoe kazi nzuri zaidi na pia Sera ielekezwe katika kuboresha teknolojia ili wasanii wafaidike.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (kulia) akiongea waandishi wa habari kuhusu vyombo vya habari (tekevision na Redio) kuanza kulipia mirahaba kwa wasanii wa muziki leo jijini Dar es Salaam. Mhe Mwijage aliwasisistiza wasanii kwenda COSOTA kuandikisha kazi zao ili zitambulike na wafaidike kwa kulipwa mirahaba.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.