KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
***************************************************
Na Shamimu Nyaki.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
jamii,Jinsia,Wazee Na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo amezindua Bodi Mpya ya Wadhamini ya Taasisi ya Saratani
katika Hospitali ya Ocean Road Ambayo
itasimamia programu za elimu ya afya kuhusu Saratani.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe.
Ummy Mwalimu mbali na kutoa pongezi za
uundwaji wa Bodi hiyo amewataka
watendaji kuhakikisha wagonjwa wa Saratani wanapata huduma bora, ushauri wa namna ya kuzuia magonjwa ya
Saratani, kufanya utafiti wa magonjwa ya
Saratani kwa kushirikiana na wadau
wengine wa ndani na Nje kwa kuwa Taasisi hiyo imeanzishwa ili kuwasaidia
wagonjwa hao.
“Tumieni uzoefu wenu,vipaji vyenu, na
taaluma zenu katika kutoa huduma kwa kuwa Taasisi hii inategemewa na watu
wote”Alisema Mhe.Waziri.
Aidha Waziri huyo amewahakikishia
watandaji wa Bodi hiyo kwamba atashirikiana
nao kwa karibu zaidi katika kufanikisha ugojwa wa Saratani unatokomea au
kupungua kwa vile Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) inaonyesha kuwa Tanzania ina jumla ya wagonjwa 33,884 lakini wanaopata huduma ni Wagojwa 3000 ambao ni sawa na asilimia 16 tu.
Mhe Ummy amesema atahakikisha Taasisi hiyo
inatengewa fedha za kutosha ili iweze kutoa huduma na kupunguza
tatizo la ugonjwa wa Saratani hapa nchini kwa kufanya tafiti muhimu
Ktika maeneo tofauti na kutoa elimu kwa
wananchi kuhusu ugojwa huo kwa vile wananchi wengi wanagundua ugonjwa huo ukiwa
tayari umeshakuwa na athari kubwa.
Katika Hatua nyingine Mhe. Waziri
Ummy amesikitishwa na kitendo cha
Hospitali hiyo kukosa Dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa saratani kama vile
damu,dripu ambapo wagonjwa hulazimika kutafuta
huduma nje ya Hospitali hiyo tena kwa
gharama kubwa ya Shilingi 800,000 wakati Sera ya
Afya yaTaifa inasema huduma kwa wagonjwa wa Saratani hutolewa bure.
Kutokana na Ukosefu wa dawa hizo
Waziri Ummy ameitaka Bohari kuu ya dawa
(MSD) kuandaa maelezo kuhusu ukosefu wa
Dawa za Saratani katika hospitali na waharakishe wanatafuta njia ya kupatikana kwa
dawa hizo haraka ili wagonjwa Wapate
huduma na kuwaagiza watendaji
kuwashawishi wagonjwa na wananchi kwa
ujumla kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) ambao utawasaidia katika
matibabu.
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo ya Ocean Road Bw Hamisi Diyenga alitoa ufafanuzi kuhusu ukosefu wa dawa za
kupunguza Makali ya ugonjwa wa Saratani kwamba umetokana na uhaba wa Bajeti,ukosefu
wa Mashine za kutosha kwa ajii ya matibabu ya mionzi kwa wagonjwa kwakuwa silimia 90 ya wagonjwa
wa Saratani wanatibiwa kwa mionzi.
Kaimu Mkurugenzi huyo amemueleza Waziri huyo wa Afya jitihada wanazozifanya kuhakikisha wanatoa
huduma bora kwa wagonjwa kwamba
wametenga shilingi Bilion 15 kwa ajili ya kununua mashine za kutoa huduma ya
mionzi pamoja na kukarabati mashine ambazo zimeharibika.
“Huduma ya mionzi kwa wagonjwa wa
Saratani ni muhimu sana katika kumpa
nafuu hivyo tunalazimika kutoa kwa wale
wanaohitaji huduma za dharura tuu” Alisema Mkurugenzi huyo.
Katika ziara hiyo Mhe. Waziri
aliwatembelea wagojwa waliolazwa,akakagua Mashine za mionzi pamoja na jengo linalojengwa kwa ajili ya
kutoa huduma ya mionzi kwa wagonjwa wa Saratani ambapo huduma hiyo inapatikana
hospitali ya Ocean Road pekee.
No comments:
Post a Comment