TIMU ya Simba ya jijini Dar es Salaam, leo tena imeendeleza wimbi la ushindi wa pili mfululizo ikiwa na Kocha wake mpya Jackson Mayanja, baada ya kuibanjua JKT Ruvu mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa.
Mabao hayo yalifungwa na Hamis Kiiza kwa mkwaju wa penati na Dani Lyanga katika kipindi cha pili.
Kwa ushindi huo sasa Simba wamefikisha jumla ya Pointi 33, huku wakiendelea kubaki katika nafasi ya tatu chini ya Yanga SC na Azam Fc ambao nao wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mgambo JKT ugenini kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo.
Kwa ushindi huo wa Azam Fc sasa wamefikisha jumla ya Pointi 39 na kurejea tena kuongoza usukani wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara wakiwa juu ya Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo Yanga SC, wenye Pointi 36 ambao nao wanashuka dimbani kesho kukipiga na Maji Maji ya Songea, kwenye Uwanja wa Taifa Dar.
MATOKEO YA MECHI ZA LEO
Januari 20, 2016
JKT Ruvu 0-2 Simba SC
Mgambo JKT 1-2 Azam FC
Stand United 2-1 Toto Africans
Ndanda FC 4-1 Mbeya City
Prisons 2-1 Coastal Union
JKT Ruvu 0-2 Simba SC
Mgambo JKT 1-2 Azam FC
Stand United 2-1 Toto Africans
Ndanda FC 4-1 Mbeya City
Prisons 2-1 Coastal Union
RATIBA LIGI KUU BARA KESHO
Januari 21, 2016
Yanga SC Vs Majimaji
Mwadui FC Vs Kagera Sugar
African Sports Vs Mtibwa Sugar
Yanga SC Vs Majimaji
Mwadui FC Vs Kagera Sugar
African Sports Vs Mtibwa Sugar

No comments:
Post a Comment