TIMU ya Al Ahly imesonga mbele michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa jumla wa 3-2 katika mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 Bora uliopigwa kwenye Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria baada ya awali kulazimisha sare ya 1-1 Uwanja wa Dar es Salaam wiki mbili zilizopita.
Bao la pili la Abdallah Said la dakika ya tano katika muda wa nyongeza baada ya kukamilika kwa dakika 90 za kawaida za mchezo akimalizia krosi ya Walid Soliman lilitosha kuwafungashia virago Yanga walioonekana kukomaa na kuwachanganya zaidi Waarabu hao, walioanza kuwachanganya wachezaji wa Yanga kwa vurugu za ugomvi.
Yanga walipata bao la kuswazisha katika dakika ya 66 kupitia kwa Donald Ngoma, akimalizia krosi murua iliyopigwa na beki wa kulia, Juma Abdul, wakati bao la kwanza la Al Ahly lilifungwa na kiungo Hossam Ghaly aliyeunganisha kwa kichwa kona ya Ahmed Fathi dakika ya 51.
Kwa ushindi huo wa Al Ahly, Yanga SC imetolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Aidha baada ya kutolewa katika mashindano hayo sasa Yanga, inatarajia kucheza na moja ya timu zilizofuzu Kombe la Shirikisho kuwania nafasi ya kupangwa kwenye makundi.
CAF CONFEDERATIONS CUP 2ND ROUND VICTORS ARE: -
Sagrada Esperanca ( Angola)
Misr+ El -Makasa ( Egypt)
CF Mounana( Gabon)
FUS Rabat ( Maroc)
Esperance de Tunis ( Tunisia)
Stade Gabesien ( Tunisia
TO MEET EITHER OF THE FOLLOWING FROM CAF CHAMPIONS LEAGUE 2ND ROUND LOSES: -
Mo Bejaia ( Algeria)
TP Mazembe ( DR Congo)
AL - Ahli Tripoli( Libya)
Stade Malien ( Mali)
Mamelodi Sundowns ( South Africa )
AL - Merreikh ( Sudan)
Young Africans ( Tanzania)
Yanga, hii ni mara ya pili kufikia hatua hiyo baada ya mwaka 2007. ambapo mwaka huo Yanga ilifungwa mabao 3-0 na Esperance ya Tunisia katika hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kutoa sare 0-0 jijini Mwanza nchini Tanzania katika mchezo wa marudiano kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho na ilitolewa na El Merreikh ya Sudan, ikitoa sare ya 0-0 Mwanza na kufungwa 2-0 Khartoum.
Yanga inaweza kukutana tena na Esperance ambayo imeitoa Azam FC ya Tanzania jana kwa jumla ya mabao 4-2, ikishinda 3-0 katikamchezo wa marudiano wa jana usiku Tunis baada ya kufungwa 2-1 jijini Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza.
No comments:
Post a Comment