Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe.
George Simbachawene akizungumza katika hafla ya kuwaapisha Wakurugenzi wa
Halmashauri za Miji, Manispaa na Wilaya 13 walioteuliwa hivi karibuni. Hafla hiyo
ilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Angella
Kairuki, Naibu Waziri Selemani Jafo, baadhi ya wakurugenzi, wafanyakazi kutoka
OR-TAMISEMI pamoja na waandishi wa habari.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na
Utawala Bora, Mhe. Angella Kairuki akiongea Wakurugenzi wapya mara baada ya
kuapishwa leo mjini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene. Kushoto kwa
Simbachawene ni Mkurugenzi mteule wa Halmashauri
ya Wilaya ya Kilimanjaro Bi. Butamo Nuru Ndalahwa
Baadhi
ya Wakurugenzi wa halmashauri wakisaini hati ya kiapo cha maadili ya utumishi wa
umma pamoja na ahadi ya kuwa waaminifu na wazalendo kwa nchi yao
leo katika ofisi za TAMISEMI mjini Dodoma mbele ya Katibu Msaidizi Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Ofisi ya Kanda ya Kati Cathlex Makawia.
Baadhi
ya Wakurugenzi wa halmashauri wakisaini hati ya kiapo cha maadili ya utumishi wa
umma pamoja na ahadi ya kuwa waaminifu na wazalendo kwa nchi yao
leo katika ofisi za TAMISEMI mjini Dodoma mbele ya Katibu Msaidizi Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Ofisi ya Kanda ya Kati Cathlex Makawia.
*******************************************************
Na Nasra Mwangamilo- Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (OR-TAMISEMI)
Mhe. George Simbachawene amewaasa
Wakurugenzi wapya kusimamia mapato ya ndani katika halmashauri zao ili waweze
kutekeleza miradi ya maendeleo na kuwahudumia wananchi.
Waziri Simbachawene amesema hayo leo mjini
Dodoma wakati wa hafla ya kuwaapisha Wakurugenzi wapya 13 walioteuliwa na Mhe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
iliyofanyika katika jengo la Mkapa, Ofisi ya Rais, Tawala za Mkoa na Serikali
za Mitaa mjini Dodoma. Pamoja na kuapishwa, Wakurugenzi hao walikula kiapo cha
maadili ya utumishi wa umma pamoja na ahadi ya kuwa waaminifu na wazalendo kwa
nchi yao.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Waziri Simbachawene
alisema Wakurugenzi hao wanawajibu wa kusimamia mikataba iliyopo, iliyopita na
itakayoingiwa na halmashauri zao ikiwa
ni pamoja na kuzingatia masharti ya mikataba hiyo wakati wa utekelezaji wake.
Aidha, aliwahimiza kuwa wawajibikaji kwa mamlaka waliyonayo kwa kufuata sheria,
kanuni na taratibu zilizowekwa kikatiba.
“Kuanzia
leo mnaitwa viongozi, unapokuwa kiongozi unalazimika kuishi kwa namna tofauti
kabla ya kuapishwa kuwa kiongozi, eneo mnaloenda kufanya kazi ni muhimu na
mnaenda kuongoza taasisi na mnaenda kuwahudumia wananchi moja kwa moja” alisema
Simbachawene.
Waziri Simbachawene amewaeleza Wakurugenzi
hao kuwa unapozungumzia kuondoa umasikini wa wananchi, Mkurugenzi ndiye
anayebeba bendera na dhamana ya kusimamia sekta zote ndani ya halmashauri
ikiwemo afya, kilimo, elimu, maji, uvuvi ambazo zitawaletea hali bora ya maisha
ya wanachi hao.
Katika
kuyatekeleza majukumu hayo, Waziri Simbachawene amewahimiza wakurugenzi
hao kufanya kazi na Wizara zote kwa kufutata sera mbalimbali na miongozo
inayotolewa na viongozi wakuu wa nchi akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.
Aidha,
Waziri
Simbachawene
amewataka Wakurugenzi hao kutembelea maeneo yao katika halmashauri zao badala
ya kukaa ofisini kuanzia tarehe 1 hadi 30 kila mwezi ili kujionea changamoto
zinazowakabili wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
“Tokeni
ofisini na tembeleeni maeneo yenu, mna mambo mengi ya kufanya, ni lazima uwajue
wananchi, viongozi unaofanya nao kazi, taasisi na watumishi wako kwa takwimu
ikiwezekana kwa majina” alisisitiza Waziri Simbachawene.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Utumishi na Utawala Bora Angellah Kairuki amewataka Wakurugenzi hao
wafuatilie na kusimamia miradi ya maendeleo iliyopo ndani ya halmashauri zao
kwa kuzingatia matumizi sahihi ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya kutekeleza miradi
hiyo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Kuhusu watumishi hewa, Waziri Kairuki
amesema kuwa hadi sasa wamebainika watumishi hewa 17,102 tangu kuanzishwa zoezi
hilo Machi mosi mwaka huu na kuwaasa wakurugenzi hao kufuatilia watumishi ndani
ya halmashauri zao ili kuondokana na dhana ya kuwa na watumishi hewa ndani ya
halmashauri zao.
Ili kuwa na taarifa sahihi, Waziri Kairuki
amewataka Wakurugenzi hao watumie mifumo sahihi ili kutoa taarifa sahihi za
watumishi na kuondoa dhana ya watumishi hewa ndani ya halmashauri zao.
Kwa upande wao Mkurugenzi mpya wa halmashauri ya wilaya ya Bukoba
Mwantumu Dau na Frank Bahati wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe wamemshukuru
Rais kwa kuwateua na kuhahidi kutomuangusha ambapo na watawatumikia wananchi
kwa nguvu zao zote katika kuwaletea maendeleo.
Wakurugenzi 13 wa Halmashauri za Manispaa,
Mji na Wilaya walioapishwa na Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya
Vingozi wa Umma, Ofisi ya Kanda ya Kati Cathlex Makawia ni pamoja na Godwin
Emmanuel Kunambi Manispaa ya Dodoma, Elias R. Ntiruhungwa Mji waTarime,
Mwantumu Dau Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Frank Bahati Halmashauri ya
Wilaya ya Ukerewe, Hudson Stanley Kamoga Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Mwailwa
Smith Pangani Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Godfrey Sanga Halmashauri ya
Wilaya ya Mkalama na Yusuf Daudi Semuguruka Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga.
Wakurugenzi wengine ni Bakari Kasinyo
Mohamed Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Juma Ally Mnweke Halmashauri ya
Wilaya ya Kibondo, Butamo Nuru Ndalahwa
Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Waziri
Mourice Halmashauri ya Wilaya ya Karatu na
Fatma Omar Latu Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment