Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh.
George Simbachawene akizungumza wakati wa mkutano wa kuzindua Bodi mpya ya Mikopo ya Serikali
za Mitaa leo mjini Dodoma.
Baadhi
ya wajumbe wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa wakifuatilia uzinduzi wa Bodi
hiyo katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mkapa leo mjini Dodoma.
Naibu Katibu mkuu anayeshughulikia elimu kutoka Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Bw. Benard Makali akizungumza katika mkutano wa kuzindua bodi mpya ya Mikopo ya
Serikali za Mitaa katika Jengo la Mkapa mkoani Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa wakifuatilia uzinduzi wa Bodi hiyo katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mkapa leo mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. George Simbachawene akikata utepe wa nyaraka muhimu zinazohusu
Bodi, katika mkutano wa kuzindua bodi mpya ya Mikopo ya Serikali za Mitaa katika
Jengo la Mkapa mkoani Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. George Simbachawene kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya mikopo na baadhi ya watumishi wa bodi hiyo katika mkutano wa kuzindua bodi mpya ya Mikopo ya Serikali za Mitaa katika Jengo la Mkapa mkoani .
***********************************************************
Na,
Nasra Mwangamilo
Bodi
ya Mikopo ya Serikali za Mitaa yatakiwa kuongeza fursa itakayoziwezesha
Serikali za Mitaa nchini kupata fedha za kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi hasa
katika miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma za kijamii.
Wito
huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI) Mh. George Simbachawene alipokuwa akizindua rasmi Bodi hiyo leo
mjini Dodoma.
“Natambua
kuwa nyenzo muhimu za kutekeleza majukumu ya Bodi ni rasilimali fedha ambazo zinatakiwa
zipatikane kupitia vyanzo mbalimbali ambavyo vimeainishwa kwa mujibu wa sheria,
kifungu cha 62 cha Sheria ya Bodi ya mikopo
kinataja njia mbalimbali ikiwemo kupata fedha kama zitavyoainishwa na Bunge
kwa madhumuni ya kuendesha shughuli za Bodi”.Aalisema Mh. Simbachawene.
Aidha
alisisitiza kuwa Bodi hiyo ijitahidi kusimamia kwa ukaribu zaidi uwekezaji kwa kuelekeza
rasilimali kwenye vitega uchumi vyenye faida kubwa ikiwa ni njia mojawapo ya kujiongezea
mapato huku ikiwa na lengo la kuhakikisha inatoa mikopo kulingana na makubaliano
baina ya Bodi na Halmashauri husika.
Pia
aliwataka wa jumbe wa Bodi kusimamia kwa ukaribu utendaji wa Bodi hiyo na kuhakikisha
kwamba hesabu zinatunzwa vizuri na taarifa zinatolewa kwa wakati hii ni pamoja na
kuweka amana za muda maaalumu kwenye mabenki, umiliki wa hisa katika mabenki,
kodi ya pango kutoka kwenye nyumba zinazomilikiwa na Bodi pamoja na malipo ya riba
kutoka kwenye mikopo.
“Nitumie
nafasi hii kusisitiza kwamba nanyi kama wa jumbe wa bodi hii lazima kusimamia kwa
ukaribu utendaji wa bodi ya mikopo na kuhakikisha kwamba hesabu zinatunzwa vizuri,
Ni vizuri taarifa za bodi zipatikane kwa wakati nakuwasilishwa mbele ya bodi na
kujadiliwa kwa wakati”. Alisisitiza Waziri.
Kukosekana
kwa mwamko wa kimaendeleo miongoni mwa baadhi ya viongozi na watendaji wa Halmashauri
hivyo kuna umuhimu wa bodi hii mpya kusaidia kuchochea ubunifu wa kimaendeleo ili
Halmashauri ziinue miradi bora inayokopesheka na yenye faida kubwa.
No comments:
Post a Comment