Naibu
Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura
(kushoto) akizungumza na Wadau wa Lugha ya Kiswahili (hawapo pichani) wakati wa
kikao na wadau hao kujadili changamoto zinazokabili Tasnia ya Lugha nchini na
kuzipatia ufumbuzi leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Lugha
Hajjat Shani Kitogo
Mkurugenzi Msaidizi Lugha Hajjat Shani Kitogo akifafanua jambo wakati wa kikao na wadau wa Lugha ya Kiswahili kujadili changamoto zinazokabili Tasnia ya Lugha nchini na kuzipatia ufumbuzi leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura
Mwandishi wa Vitabu vya Riwaya Bw. Adam Shafi (aliyesimama) akichangia mada wakati wa kikao na wadau wa Lugha ya Kiswahili kujadili changamoto zinazokabili Tasnia ya Lugha nchini na kuzipatia ufumbuzi leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mmiliki wa kampuni ya machapisho ya Mkuki na Nyota Bw. Walter Bgoya
Wadau mbalimbali wa Lugha ya Kiswahili wakijadiliana wakati wa kikao na Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (kushoto) kujadili changamoto zinazokabili Tasnia ya Lugha nchini na kuzipatia ufumbuzi leo Jijini Dar es Salaam.
Mshairi mama Mipango akiimba shairi la kuipongeza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kusimamia vizuri Lugha ya Kiswahili katika kuikuza na kuieneza wakati wa kikao na wadau wa Lugha ya Kiswahili kujadili changamoto zinazokabili Tasnia ya Lugha nchini na kuzipatia ufumbuzi leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na Wadau wa Lugha ya Kiswahili wakati wa kikao na wadau hao kujadili changamoto zinazokabili Tasnia ya Lugha nchini na kuzipatia ufumbuzi leo Jijini Dar es Salaam. Kulia waliokaa ni Mkurugenzi Msaidizi Lugha Hajjat Shani Kitogo na kushoto waliokaa ni Mjumbe kutoka Idara ya Lugha na Fasihi Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Bibi. Gertrude Joseph. Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM
*********************************************************
Na: Genofeva
Matemu – WHUSM
Wadau
wa Lugha ya Kiswahili nchini wamepongezwa kwa kazi kubwa na nzuri wanazozifanya
za kukuza, kueneza, kuimarisha na kuendeleza lugha ya Kiswahili kwani wamekifanya
Kiswahili kuwa lugha yenye mawasiliano mapana katika nchi za Afrika Mashariki,
Afrika na Dunia nzima.
Hayo
yamesema na Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Anastazia James Wambura wakati wa kikao na wadau hao kujadili changamoto
zinazokabili Tasnia ya Lugha nchini na kuzipatia ufumbuzi leo Jijini Dar es
Salaa.
“Vyama
mbalimbali vya kukuza na kueneza Lugha ya Kiswahili nchini kwa kushirikiana na
wadau mbalimbali mmekua kichocheo kikubwa cha kuendeleza lugha ya Kiswahili na
kuisambaza kwa kasi hata kuweza kuvuka mipaka ya Tanzania” amesema Mhe.
Anastazia.
Mhe.
Anastazia amewataka wadau wa Lugha ya Kiswahili kushiriki vema katika mijadala
itakayokua inaandaliwa ya lugha hiyo ili waweze kutoa maoni na mapendelkezo fahafu
yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali, Taasisi, Asasi na vyama
mbalimbali vya wadau wa lugha ya Kiswahili nchini.
Kwa
upande wake Mkuregenzi kutoka Chama cha Kiswahili na Sanaa (KINASA) Bw.
Mutalemwa Jason ameiomba serikali kuhakikisha kuwa utamaduni wa Vilabu vya
Kiswahili kwa shule za msingi na sekondari unarejeshwa ili kutoa fursa nzuri
kwa wanafunzi kukutana na kujadili misamihati mbalimbali ya Kiswahili.
Naye
Naibu Katibu Mkuu kutoka Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA) ameviomba vyombo
vya habari nchini kusaidia kurusha mashairi yanaimbwa na wadau wa lugha ya
Kiswahili kwani kwa kufanya hivyo watawezesha misamihati ya lugha ya Kiswahili
kuenea kwa kasi ndani na nje ya nchi.
Tangu
tulipopata uhuru mwaka 1961 masuala yahusuyo Lugha katika nchi yetu yamezingatiwa kama
kipengele muhimu katika Sera ya Utamaduni ya mwaka 1997, Serikali ya awamu ya
tano imezingatia umuhimu mkubwa wa kuwa na Sera ya Taifa ya Lugha ambayo ni
muongozo dhabiti inayosimamia masuala yote yanayohusu Lugha nchini ambapo kwa
sasa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inaendelea na mchakato wa uandaaji
wa rasimu ya Sera ya Taifa ya Lugha katika hatua ya ukusanyaji wa maoni ya
wadau wa Lugha hiyo.
No comments:
Post a Comment