Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akimimina mchanganyiko
wa mahitaji ulioandaliwa kwa ajili ya kutengeneza chaki katika moja ya mashine
ya kutengeneza chaki hizo kabla ya
kuzindua rasmi kiwanda cha chaki jana katika Halmashauri ya Maswa Mkoani
Simiyu. katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka na kushoto ni
kijana kutoka Maswa Youth Famili Bibi. Brenda Kasea.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe.
Jenista Mhagama akisalimiana na baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Maswa baada ya kuwasili katika Halmashauri hiyo jana Mkoani Simiyu kabla ya
kwenda kufungua kiwanda cha chaki kinachoendeshwa na vijana wa Maswa Youth
Family.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe.
Jenista Mhagama (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Maswa Dkt. Seif
Shekalaghe (aliyesimama kushoto) baada ya kuwasili katika Halmashauri hiyo jana
Mkoani Simiyu kabla ya kwenda kufungua kiwanda cha chaki kinachoendeshwa na
vijana wa Maswa Youth Family. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akipokea taarifa fupi ya Wilaya ya Maswa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Seif Shekalaghe (kushoto) baada ya kuwasili katika Halmashauri hiyo jana Mkoani Simiyu kabla ya kwenda kufungua kiwanda cha chaki kinachoendeshwa na vijana wa Maswa Youth Family.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) akizungumza na viongozi kutoka Mkoa wa Simiyu na Halmashauri ya Maswa baada ya kuwasili katika Halmashauri hiyo jana Mkoani Simiyu kabla ya kwenda kufungua kiwanda cha chaki kinachoendeshwa na vijana wa Maswa Youth Family.
******************************************************
Na:
Genofeva Matemu – WHUSM
Vijana
nchini wametakiwa kuiga mfano wa vijana wa Maswa Youth Family kuunganisha nguvu
zao kuibua miradi yenye tija kwani heshima ya kijana ni kujitengemea na
kulitegemeza taifa lake.
Hayo
yamesema na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ufunguzi wa Kiwanda cha Chaki
Jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu.
“Vijana
wa Maswa Youth Family ni mfano bora wa kuigwa kwani ni vijana waliojitambua na
kutambua yakua umoja ni nguvu hivyo kuchagua fungu lililo jema na kuwa mfano
bora kwa wana Maswa na taifa kwa ujumla” alisema Mhe. Jenista.
Aidha
Mhe. Jenista amemuagiza Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana kuwakopesha
tena vijana wa Maswa Youth Family shilingi milioni thelathini kutoka katika
mfuko wa vijana ili kiwanda hicho kiweze kukua kwa haraka na kuzalisha chaki kwa
wingi hivyo kuweza kuzuia soko la chaki zinazotoka nje ya nchi.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa kiwanda cha chaki Wilayani Maswa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Mhe. Anthony Mtaka amesema kuwa hadi sasa uzalishaji wa chaki unaofanywa na
kiwanda kidogo cha Maswa Youth Family unatosheleza mahitaji ya chaki kwa shule
zote za Mkoa huo na kuzipiga marufuku shule zote mkoani hapo kununua chaki nje
ya Mkoa wa Simiyu.
“Simiyu
imedhamiria kuionyesha nchi kuwa sisi ngozi nyeusi tunaweza tukaibua miradi,
tukajenga uwezo na baadaye tukazalisha kwa kuiendeleza kauli mbiu ya mkoa wetu
ya bidhaa moja wilaya moja ambayo baadaye itashuka hadi kuwa bidhaa moja kijiji
kimoja na kulifanya taifa letu kuwa taifa la viwanda” alisema Mhe. Mtaka.
Aidha
Naibu Waziri Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde amesema kuwa Mkoa wa
Simiyu umekua wakwanza kuiishi kwa vitendo falsaga ya bidhaa moja wilaya moja na
kuahidi kuiunga mkono falsafa hiyo kujitolea kuwa balozi wa Chaki
inayotengenezwa na Maswa Youth Family ili kuweza kuitangaza nchi nzima.
Naye
Mwenyekiti wa Maswa Youth Family Bw. Kelvin Steven amesema kuwa kiwanda hicho
kina uwezo wa kuzalisha chaki 38,400 kwa saa sawa na katoni 16 na iwapo
uzailishaji utafanyika kwa saa nne kiwanda kitazalisha katoni 128 kwa siku na
uzalishaji huo kwa siku 20 unategemewa kuwa katoni 2560 ambapo mahitaji kwa
mwezi kwa Wilaya inakadiriwa kuwa katoni 157 hivyo kuwa na zaidi ya katoni 2403
ambazo zitauzwa maeneo mengine.
Mradi
huu umegharimu jumla ya shilingi 37,967,522 kati ya fedha hizo shilingi
30,967,522 ni mchango wa Halmashauri na shilingi 70,000,000 ni mchango wa
kikundi uliotokana na fedha za mkopo waliopewa kutoka Mfuko wa Maendeleo ya
Vijana.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe.
Jenista Mhagama (katikati) akiangalia chaki alizozitengeneza katika kiwanda cha
Maswa Youth Family kabla ya kukizundua rasmi kiwanda hicho jana katika
Halmashauri ya Maswa Mkoani Simiyu. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Mhe. Anthony Mtaka na kulia ni kijana kutoka Maswa Youth Family Bw. Razaro
Zabroni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) kwa
kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka (kulia) na Mkuu wa
Wilaya ya Maswa Dkt. Seif Shekalaghe (kushoto) kukata utepe kuzindua rasmi
kiwanda cha chaki cha Maswa Youth Family
jana katika Halmashauri ya Maswa Mkoani Simiyu.
Picha ya psmoja
No comments:
Post a Comment