Benny
Mwaipaja, MoFP, Washington
DC, Marekani
SERIKALI
ya Japan, kupitia Shirika lake la Maendeleo-JICA, imeahidi kuongeza kiwango cha
ruzuku kwa serikali ya Tanzania ili kufadhili miradi mbalimbali ikiwemo kilimo,
Maji, miundombinu ya barabara na huduma nyingine za jamii ili kuisaidia kufikia
maendeleo yaliyokusudiwa kwa wananchi wake.
Ahadi
hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan-JICA, Hiroshi
(Hiro) Kato, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango,
Dkt. Philip Mpango, Jijini Washington DC, nchini Marekani.
“Kabla
ya mwaka 2013 tulikuwa tunatoa ruzuku ya dola milioni 1 kwa Tanzania kila
mwaka, lakini kuanzia mwaka 2013 tumeongeza kiwango hadi kufikia dola milioni
mia 3 kila mwaka na tunatarajia kuongeza kiwango hicho siku za hivi karibuni”
aliongeza Makamu huyo wa Rais wa JICA
Kato
amesema kuwa Tanzania na Japan ni marafiki wa muda mrefu na kwamba nchi hiyo
itaendelea kuisaidia kwa kutekeleza miradi mbalimbali yenye kuleta tija kwa
uchumi wa nchi na maisha ya watanzania kwa ujumla.
“Hivi
sasa tunataka kuanza kutekeleza awamu nyingine ya mradi wa kilimo cha
umwagiliaji cha zao la mpunga ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo ambalo ni
muhimu sana” Aliongeza Kato.
Amesema
kuwa Japan pia imeamua kuongeza kiwango cha ufadhili kwa Bara la Afrila kutoka
Dola Milioni 13 ambazo nchi hiyo ilikuwa ikitoa kwa kipindi cha miaka mitano
kuanzia mwaka 2013 hadi kufikia dola elfu 30 kwa mwaka kuanzia mwezi Agosti,
2016 kwa kipindi cha miaka 3 ijayo.
Amesema
pia kuwa ili kuwajengea uwezo na ujuzi vijana wa kiafrika, Japan imeanzisha
program ya kutoa elimu ambapo hivi sasa vijana 60 kutoka nchi mbalimbali za
kiafrika wamepelekwa nchini humo kujifunza kwenye vyuo vilivyoko huko na
watapelekwa kwenye kampuni na mashamba makubwa yanayojihusisha na kilimo ili
waweze kupata uzoefu na kuwa chachu ya mabadiliko watakaporejea katika nchi
zao.
Akiongea
na Makamu huyo wa Rais wa Shirila la Maendleo la Japan-JICA, Waziri wa Fedha na
Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameishukuru Japan kwa kuisaidia Tanzania katika
Nyanja mbalimbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Ametaja
baadhi ya miradi ambayo nchi hiyo inafadhili nchini Tanzania kuwa ni ujenzi wa
barabara ya Arusha hadi Holili hadi Taveta nchini Kenya, Ujenzi wa barabara ya
Juu (Flyover) ulioanza eneo la Tazara ili kupunguza msongamano Jijini Dar es
salaam, miradi ya maji na kilimo cha umwagiliaji.
“Asilimia
75 ya wananchi wetu wanategemea kilimo kwahiyo uamuzi wa Japan wa kuwekeza
fedha nyingi kwenye miradi ya kilimo cha umwagiliaji ni jambo tunalolipongeza
kwasababu kilimo kitakuwa na tija na kitaendeshwa kibiashara” Alisema Dkt.
Mpango.
Ameishukuru
pia serikali ya Japan kwa kufanya utafiti na upembuzi yakinifu wa mradi wa
kudhibiti mafuriko ya mto Kondoa, eneo la mkoa wa Morogoro ili kudhibiti mto
huo usiharibu miundombinu ya reli ya kati.
“Mradi
huu ni muhimu sana kwasababu serikali imekuwa ikiingia hasara karibu kila mwaka
kukarabati njia hiyo ya reli baada ya kusombwa na maji, hivyo tunaishukuru
Japan kwa kutusaidia kufanya utafiti huo ambao utasaidia kukabiliana na hali
hiyo” aliongeza Dkt. Mpango
Ameahidi
kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga kukusanya kodi na kuziba mianya ya
upotevu wa fedha za serikali ikiwemo kuanzisha mahakama maalumu ya kushughulika
na mafisadi ili kuleta nidhamu katika utumishi wa umma.
No comments:
Post a Comment