Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe.
Jenista Mhagama kulia akicheza ngoma na kikundi cha ngoma kilichokua
kikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha maziwa Meatu Milk jana katika
Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu. Kushoto ni Mkurugenzi Maendeleo
ya Vijana Bw. James Kajugusi na wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Simiyu Dkt. Titus Kamani.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe.
Jenista Mhagama (wapili kushoto) akiangalia moja ya jiko la kuandalia maziwa
kabla ya kuyasindika alipotembalea kiwanda hicho wakati wa uzinduzi wa kiwanda
cha Meatu Milk jana katika Halmashauri ya Meatu Mkoani Simiyu. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) akiangalia moja ya kifungashio cha maziwa ambacho tayari kimeshawekewa maziwa wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha Meatu Milk jana katika Halmashauri ya Meatu Mkoani Simiyu. Wapili kushoto ni Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico
: Baadhi ya
vijana wa Meatu Milk akimsikiliza kwa makini Mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa
kiwanda hicho jana katika Halmashauri ya Meatu Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe. Rachel Kasanda akizungumza na vijana wa Meatu Milk (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho jana katika Halmashauri ya Meatu Mkoani Simiyu.
Waziri
wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar Mhe. Moudline Castico (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa
kiwanda hicho jana katika Halmashauri ya Meatu Mkoani Simiyu. Kushoto ni Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe.
Jenista Mhagama na katikati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dkt. Titus
Kamani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (aliyesimama) akizungumza na vijana wa Meatu Milk (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho jana katika Halmashauri ya Meatu Mkoani Simiyu. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dkt. Titus Kamani.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe.
Jenista Mhagama (kushoto) akimpa zawadi ya gudulia la maziwa yanayotengenezwa
na Vijana wa Meatu Milk Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na
Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico (kulia) wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho jana
katika Halmashauri ya Meatu Mkoani Simiyu.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe.
Jenista Mhagama (kushoto aliyesimama) akipokea mchango wa kuchangia uendelezaji
wa Meatu Milk kutoka kwa Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi
wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho jana katika Halmashauri ya Meatu Mkoani
Simiyu.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe.
Jenista Mhagama akimkabidhi Mkurugenzi wa Meatu Bw. Fabian Manoza Said (kulia)
zaidi ya shilingi milioni nne zilizokusanywa wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha
Meatu Milk kuendeleza kiwanda hicho jana katika Halmashauri ya Meatu Mkoani
Simiyu.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule ya sekondari Meatu wakifuatilia matukio yaliyokua yakiendelea wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha Meatu Milk jana katika Halmashauri ya Meatu Mkoani Simiyu.
Wananchi
wa Meatu wakimsikiliza mageni rasmi (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa
kiwanda cha Meatu Milk jana katika Halmashauri ya Meatu Mkoani Simiyu.
Picha na:
Genofeva Matemu – WHUSM, Simiyu
*************************************************
Na:
Genofeva Matemu – WHUSM, Simiyu
Halmashauri
ya Wilaya ya Meatu imeombwa kuwatengenezea mfumo wa kibiashara vijana wa Meatu
Milk ili waweze kuboresha na kuendeleza bidhaa ya maziwa yanayotengenezwa na
kiwanda hicho.
Rai
hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea kiwanda Meatu
Milk na kufungua jiwe la uzinduzi wa mradi wa kusindika maziwa jana katika
Halmashauri ya Meatu Mkoani Simiyu.
Mhe.
Jenista amesema kuwa mradi wa usindikaji maziwa ni mradi utakaowavuta wafugaji
wengi kuondokana na tatizo la kuangaika na mifugo yao kwa sababu soko la maziwa
litakua la uhakika hivyo kupanua uchumi wa Wilaya ya Meatu.
“Twendeni
tukafungue matendo kwa vijana wa Tanzania tuwaondoe katika mitazamio ya fikra
hafifu na kuwapeleka katika kujitegemea ili wajenge taifa letu na kuondokana na
dhana ya umasikini waliyoikumbatia kwa muda mrefu” alisema Mhe. Jenista.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony
Mtaka amemwambia Mhe. Jenista kuwa hatamualika Simiyu kufungua makongamano na
warsha za ujasiriamali bali ataendelea
kumualika katika Mkoa wake kwa ajili ya kufungua viwanda vingine vya
vijana kwani mkoa umejipanga kuwa na viwanda vya kutosha vitakavyozalisha
malighafi zote zinazopatikana Mkoani Simiyu.
Mhe.
Mtaka amewaomba wana Meatu na wananchi wote wa Simiyu kuwa na uthubutu wa
kubuni miradi endelevu ili waweze kujivunia vya kwao kwani Mkoa umejichagua
kuwa pacha wa kutekeleza Ilani ya uchaguzi sambamba na Rais Mhe. John Pombe
Magufuli na kuweza kuiongoza nchi kufukia malengo ya Ilani ya Chama tawala kwa
vitendo.
Aidha
Mwenyekiti wa Meatu Milk Bibi. Lightness Benedictor amesema kuwa mradi
umegharimu kiasi cha shilingi 34,903,000 ambapo shilingi 10,000,000 ni michango
ya wanachama kutoka kwenye gawio ya fedha za mkopo uliotolewa na Wizara kutoka
Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na kiasi cha shilingi 24,902,000 ni mkopo kutoka
kwenye asilimia tano ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya fedha zilizotengwa
kuwezesha vijana.
Mradi
wa Meatu Milk unatekelezwa chini ya mpango mkubwa wa kiuchumi wa Mkoa wa Simiyu
wa kuanzisha bidhaa moja kwa Wilaya moja ili kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya
Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015/2020 ya kuwa na Tanzania ya viwanda.
No comments:
Post a Comment