Mwanasheria
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Bi. Fausta Mahenge akitoa elimu ya mpiga
kura kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria yanayosimamia chaguzi za Tanzania
kwa wanafunzi 743 wa Shule ya Sekondari
Kidinda wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Afisa Uchaguzi wa NEC Bw. Stephen Elisante akiwaonyesha wanafunzi wa shule ya Sekondari Kidinda fomu maalumu zinazotumika kujaza matokeo ya uchaguzi katika vituo vya kupigia kura wakati akitoa elimu ya Mpiga Kurra kwa wanafunzi wa shule hiyo, Bariadi mkoani Simiyu.
Afisa Uchaguzi wa NEC Bw. Stephen Elisante
akisisitiza jambo kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Kidinda wakati akitoa
elimu ya Mpiga Kurra kwa wanafunzi wa shule hiyo, Bariadi mkoani Simiyu.
Makamu
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kidinda Mwalimu Paul Susu akizungumza na wanafunzi
wa shule hiyo mara baada ya kuwakaribisha Maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
waliofika shuleni hapo kutoa Elimu ya Mpiga Kura kwa wanafunzi wapatao 743 wa
shule hiyo.
Mwanafunzi wa Kidato cha tatu wa shule ya
Sekondari Kidinda, Filipo Madeni akiwauliza swali Maofisa wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi kuhusu mfumo unaotumika kuwapata wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC),Bi. Fausta Mahenge akiwaonesha mfano wa karatasi inayotumika kupigia kura
yenye majina ya wagombea wa vyama mbalimbali wakati akitoa elimu ya Mpiga Kura
katika Shule ya Sekondari Kidinda wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
No comments:
Post a Comment