Naibu Waziri wa Elimu , Sayansi na
Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya (kulia) akikata utepe wakati uzinduzi wa
program ya JIANDALIE AJIRA inayolenga kupunguza tatizo la ajira nchini. Wengine
katika picha ni Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kimataifa wa Vijana
(IYF), Bw. William Reese (wa pili kulia), Mwenyekiti wa bodi wa Taasisi
ya Ujasiriamali na Ushindani TECC Bi. Beng’I Issa (kushoto), Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani, Bw. Sosthenes Sambua (wa pili
kushoto) na Ahmed Makbel Mkurugenzi Msaidizi wa Ajira kutoka ofisi ya Waziri
Mkuu (katikati).
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa wa Mfuko wa Kimataifa wa Vijana (IYF), Bw. William Reese, akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa program ya Jiandalie Ajira jana jijini Dar es Salaam, wengine katika picha ni Mwenyekiti wa bodi wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani (TECC) Bi. Beng’I Issa (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa (TECC) Sosthenes Sambua katikati, program hiyo ili zinduliwa na Naibu Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya kwenye ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
**********************************************************************
Na Ally Daud-MAELEZO.
Mfuko wa
Kimataifa wa Vijana( Interanational Youth Foundation) imezindua rasmi programu
mpya ya miaka mitano wa JIANDALIE AJIRA unaowalenga vijana hapa nchini kama
moja ya jitihaha za kukuwajengea vijana mafunzo ya ufundi stadi na ujasiriamali
kuondokana na tatizo la ajira .
Akizindua programu
hiyo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Technolojia ,Mhandisi Stella Manyanya
alisema program hiyo ni ukombozi mkubwa kwa vijana hapa nchini kwa kuwa
itawawezeshae kutengEneza ajira na kukuza uchumi.
“Programu
hii imekuja kutengneza vijana kuwa
wabunifu na kutengneza ajira ikiwa ni pamoja na kuajiri wengine na siyo
kuwa wasaka ajira,”na kwa kufanya hivyo taifa litapiga hatua kiuchumi,aliongeza
kusema,Mhandisi huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nyasa” alisema
Mhandisi Manyanya
Aidha
Mhandisi Manyanya aliupongeza mfuko huo wa IYF kwa kuja na mradi ambao
utatekelezwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Ujasirimali na Ushindani (TECC),
Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na Shirika lisilokuwa la kiserikali la
The MasterCard Foundation.
Mhandisi Manyanya alisema pia programu hiyo itawezesha kuwaandaa
wakufunzi wa chuo cha VETA ili waweze tumika katika kuwafundisha vijana ambao
ndio walengwa katika mradi mzima na ambao wanachangamoto kubwa ya ajira.
Mbali na
hayo Mhandisi Manyanya alikitaka chuo hicho kuendeleza na kupanua wigo wa ushirikiano
na waajiri ili kujenga nguvu kazi kukidhi matwakwa ya soko la ajira kwenda
sambana na dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.
Kwa upande
wa Rais wa IYF ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa mfuko huo Bw.William Reese
alisema mfuko wao umeandaa mpango huo kwa nchi za Tanzania na Msumbiji kwa
ajili ya kuwaandaa vijana katika elimu ya mafunzo ya ufundi stadi na uujasirimali
“Tatizo la
ajira siyo la Tanzania tu bali la dunia nzima kwa nchi zilizoendelea na ambazo
hazijaendelea”, na hitaji mipango ya pamoja, ya kidunia na yakinchi kwa
kushitrikiana na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali” alisema Bw. Reese.
Pia Mkurugenzi
wa Kanda ya Afrika IYF (Regional Director,Africa) , Bw.Mathew Breman alisema mpango
wa jiandallie ajira utaendeshwa kwa muda wa miaka mitano na unalenga kuwapatia
mafunzo ya ufundi stadi na jasirimali kwa vijana.
” Programu
hii inahusu vijana wa miaka 18 hadi 24 na watapata mafunzo na mikoa inayolengwa
ni pamoja na Dar es Salaam, Dodoma, Mtwara,na Morogoro,” na vijana 22,500
watanufaika na mradi huu, aliongeza Bw. Breman.
Aidha Bw.
Breman mradi unaletekezwa katika nchi Msumbiji ambapo kwa pamoja na
Tanzania utanufaisha vijana 30,000 kupata mafunzo ya ufundi stadi na
ujasiriamali katika kipindi hicho.
Mwenyekiti
wa Bodi wa Taasisi ya Ujasirimali na Ushindani (TECC),Bi. Issa Beng’I alisema
program hiyo ni muhimu kwa vijana.
“Tunazo
program nyingi hapa nchini Tanzania, ikiwemo kijana jiajiri, vijana wa
bodaboda,vijana wa JKT, na sasa program ya jiandalie ajira itawawezesha
kujitambua zaidi,” na kufanikiwa kwa hili ni ukombozi mkubwa kwa taiafa letu,
aliongeza kusema Bi. Issa.
Moja ya
vijana , Nuru Mungi akitoa ushuhuda wa biashara yake, alisema mafanikio
aliyoyapata katika ujasirimali yamekuja baada ya kupata mafunzo (TECC).
“
Kutokana na mafunzo haya sasa namiliki kiwanda kidogo cha kutengneza sabuni na
naamini kupitia program ya jiandalie ajira vijana wengi watanufaika na
kupanua wigo wa ujasirimali.alisema.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Ajira toka Ofisi ya Waziri Mkuu, Ahamed Makbel,alisema tatizo la
ajira hapa nchini kwa kwa sasa limefikia asilimia 10.3.
“Tatizo
hili kwa vijana limefikia asilimia 11.7 kwa vijana amabyo ni nguvu kazi
kubwa inayobeba asilimia 56 kwa nchi nzima, vijana hao wanaumri kati ya miaka
15 hadi 35.
Mfuko wa
IYF umesha fanya kazi katika mataifa zaidi ya 70 duniani ili kuweza kusaidia
vijana mbalimbali kwa ajili ya kukuza uchumi wa kijana na taifa kwa ujumla ili
kufikia uchumi wa kati.
No comments:
Post a Comment