Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel
akiongea na Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya
(MUST) alipowatembelea akiwa mmoja wa wanachuo wa mwanzao waliohitimu katika
chuo hicho ambapo awali kilijulikana na kama Taasisi ya Sayansi na Teknolojia
(MIST).
Prof. Ole Gabriel amewahimiza viongozi hao wawe msatari wa mbele katika
kusimamia taaluma na kuwajengea uwezo wanafunzi wao wajitambue na wawe na utamaduni
bora wa kufikiri kimkakati na usimamizi ili waweze kuendana na ulimwengu wa
sasa.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel
akitembelea moja ya karakana wakati wa ziara yake hivi karibuni katika Chuo
Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST). KUSOMA ZAIDI BOFYA ZAIDI
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiteta jambo na Makamu Mkuu wa Chuo
Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST) Prof. Joseph Msambichaka mara
baada ya kikao na Menejiment ya chuo hicho wakati wa ziara yake hivi karibuni
Mkoani Mbeya.
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST) Prof. Joseph
Msambichaka (katikati) akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) moja ya madaftari yake
aliyotumia wakati akisoma chuni hapo kikijulikana kama Taasisi ya Sayansi na
Teknolojia (MIST).
Moja ya vyombo vya usafiri alivyotumia Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa mwanafunzi katika Taasisi ya
Sayansi na Teknolojia (MIST) ambapo kwa sasa ni Chuo Kikuu cha Sayansi na
Teknolojia cha Mbeya (MUST).
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyevaa tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano wake na Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST) hivi karibuni mkoani Mbeya. Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Mbeya
**********************************************************
Na
Eleuteri Mangi-WHUSM, Mbeya
Viongzi
wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST) wametakiwa kuwa imara
katika kusimamia taaluma chuoni hapo na kuwajengea uwezo wanafunzi wa kujitambua
na kuwa utamaduni bora wa kufikiri kimkakati na usimamizi ili waweze kuendana
na kasi ya ulimwengu wa sasa wa sayansi na teknolojia.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amsema
hayo alipokuwa akiongea na wajumbe wa Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Sayansi na
Teknolojia cha Mbeya (MUST) hivi karibuni alipokuwa katika ziara ya kikazi
mkoani Mbeya.
Prof.
Ole Gabriel amewaambia wajumbe hao kuwa siri kubwa ya mafanikio ni pamoja na
kutimiza amri ya sita za kufikiri kimkakati na usimamizi ikiwemo kujenga
utendaji bora, kudumisha utendaji bora, kuelewa kazi za msingi wako, kujua
mshindani wako katika kazi unayofanya, kukabiliana na kasi ya Teknolojia pamoja
na kuwa wazi juu ya malengo uliyojiwekea wakati wote.
Ili
chuo hicho kifikie malengo yake, Prof. Ole Gabriel amewaambia wajumbe wa Menejimenti
ya Chuo hicho kuwa ni vema wawe na utamaduni wa kufanya tafiti mbalimbali na
usimamizi hatua ambayo itakifanya chuo hicho kuwa bora miongoni mwa vyuo vikuu
nchini kwa kutoa wananfunzi wenye ubora unaohitajika kwenye soko la ajira ndani
na nje ya nchi.
Zaidi
ya hayo, viongozi hao wameshauriwa pia kujenga utamaduni wa kuwa miongoni mwa
watu wenye fikra kubwa ambao wanania ya kutengeneza mambo yatokeee na wasiwe
watu wa wastani wenye nia lakini wanaangalia mambo yatokee wala wasiwe watu
wenye akili za kawaida wenye nia lakini wanashangaa kwanini mambo yanatokea.
Aidha,
Prof. Ole Gabriel amezitaja sifa za mtu anayefikiri kimkakati na usimamizi kuwa
ni pamoja na daima kuona fursa nje ya matatizo, kuwa na mkakati wa majadiliano,
kuripoti matatizo na ufumbuzi mbadala, pamoja na kufanya maamuzi kwa haraka na
kwa usahihi.
Kwa
upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya
(MUST) Prof. Joseph Msambichaka kwa niaba ya Menejimenti amemshukuru Katibu
Mkuu Prof. Ole Gabriel kuwajali na kuwathamini ikizingatiwa ni miongoni mwa wanachuo
wa mwanzao waliohitimu katika chuo hicho ambapo awali kilijulikana na kama
Taasisi ya Sayansi na Teknolojia (MIST).
Akitoa
taarifa fupi ya chuo, Prof. Msambichaka amesema kuwa chuo kwa sasa kina jumla ya
wanachuo 3,852 ambapo idadi ya wanachuo wa wanaume 3,236 na idadi ya wanawake
ni 616 ambao wanasoma katika sehemu nne za chuo hicho.
Sehemu
hizo ni Taasisi ya Sayansi na Teknolojia, Taasisi ya Uhandisi na Teknolojia,
Shule ya Mafunzo ya Biashara pamoja na Chuo cha Sayansi na Ualimu wa Ufundi.
No comments:
Post a Comment