Mhasibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Fungu 50 Bw. Christopher Lupama, (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa alioambatana nao wakati wa kupokea tuzo ya Taarifa Bora ya Fedha kwa mwaka 2015, katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (NBAA) kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Mwenyekiti
wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Prof. Isaya Jairo akizungumza
na Wahasibu kutoka Taasisi za umma na binafsi waliohudhuria katika hafla ya
kutoa tuzo ya Taarifa bora ya Fedha kwa mwaka 2015, katika Kituo cha Taaluma ya
Uhasibu (NBAA) kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Kamishna
Msaidizi wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Shogholo Msangi
akizungumza na Washindani wa tuzo ya Taarifa bora ya Fedha kwa mwaka 2015 kutoka
Taasisi za umma na binafsi takribani 56, katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC)
kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Baadhi
ya Maafisa walioambatana na Mhasibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Fungu 50, Bw. Christopher Lupama,
wakipeana mkono na Viongozi wa Serikali na Bodi ya NBAA baada ya kupokea tuzo ya
Taarifa bora ya Fedha kwa mwaka 2015, katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC)
kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Kamishna
Msaidizi wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Shogholo Msangi akiwa katika
picha ya pamoja na na washindi wa tuzo ya Taarifa
Bora za Fedha kwa mwaka 2015, katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (NBAA)
kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Kamishna Msaidizi wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Shogholo Msangi (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Prof. Isaya Jairo wakibadilishana mawazo wakati wa zoezi la kuwakabidhi washindi wa Tuzo ya Taarifa bora ya Fedha kwa mwaka 2015, tukio lililofanyika katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC) kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Wahasibu nchini wametakiwa
kuzingatia viwango vya uhasibu vinavyotakiwa na kukubalika kitaifa na kimataifa
wakati wa kuandaa taarifa za fedha kwa kuzingatia maslahi ya Taifa.
Wito huo umetolewa na
Kamishna Msaidizi Sera, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Shogholo Msangi,
wakati akikabidhi tuzo za Taarifa Bora za Fedha kwa mwaka 2015/2016, kwaniaba
ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dotto James tukio lililofanyika katika Kituo cha
Taaluma ya Uhasibu (APC), kilichoko Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam
Katika tukio hilo ambalo liliambatana
na kufungwa kwa Mkutano wa mwaka wa Wahasibu unaojumuisha
nchi za Afrika Mashariki, Wizara ya Fedha na Mipango, kupitia Fungu 50, imepata
tuzo ya kuandaa vitabu bora vya mahesabu vinavyokidhi viwango vilivyowekwa na
Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi (NBAA).
Bw. Msangi amesema kuwa
taarifa za fedha hutumika katika matumizi mbalimbali katika Sekta ya umma na
binafsi, hivyo iwapo taarifa hizo zitakuwa katika viwango vyenye ubora
zitaongeza imani ya wananchi kwa Serikali yao.
Amesema kuwa taarifa hizo
pia hutegemewa na wawekezaji katika kupanga maamuzi yao ya uwekezaji hapa
nchini hatua itakayosaidia nchi kufikia malengo yake ya kuwa nchi ya viwanda na
uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Bw. Pius
Maneno, amesema kuwa, kumekuwa na mafanikio makubwa katika utoaji wa taarifa za
fedha kwa upande wa Taasisi za Umma na Binafsi mwaka huo ikilinganishwa na
miaka ya nyuma.
“Mwaka uliopita Taasisi
nyingi za umma zilishindwa kufikia asilimia 75 ambacho ndicho kiwango cha chini
kabisa cha Taasisi kuingia katika ushindani wa Tuzo ya taarifa bora ya Fedha ya
mwaka, lakini kwa mwaka huo, Taasisi za Serikali zilizokidhi kiwango hicho ni
zaidi ya Asilimia 50.” Aliongeza Bw. Maneno.
Aidha, amesema kuwa katika
kutafuta mshindi wa Tuzo hiyo taasisi mbalimbali zimehusishwa ikiwemo Mamlaka
ya Bima Tanzania, Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Taasisi ya Utawala wa Fedha na
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kabla ya matokeo kuthibitishwa na Bodi ya Wahasibu
na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya
NBAA Prof. Isaya Jairo amebainisha faida za tuzo ya taarifa bora ya fedha kuwa
ni pamoja na kujenga uwazi, uwajibikaji, uadilifu na kuwa na taarifa ya fedha
yenye viwango.
Amezitaka Taasisi nyingi
kushiriki katika ushindani ili kuboresha taarifa za fedha za Mashirika yakiwemo
ya umma na binafsi, huku akitoa wito kwa Serikali kuziagiza Taasisi zake
kushiriki kikamilifu.
Miongoni mwa wizara
zilizoibuka na ushindi wa Tuzo hiyo ni Wizara ya Fedha na Mipango Fungu 50
ambapo iliwakilishwa na Mhasibu wake Mkuu Bw. Christopher Lupama kupokea Tuzo
hiyo, ambaye amebainisha kuwa Tuzo hiyo imewapa nguvu ya kuendelea kufanya
vizuri katika utoaji wa Taarifa ya Fedha yenye viwango.
Taasisi 56 zimeshiriki
kuwania tuzo hiyo inayoandaliwa kila mwaka na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na
Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).
No comments:
Post a Comment