Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Zanzibar , Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na vyombo vya habari katika eneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa wa Mjini Magharibi ambalo matendo ya uhalifu ikiwepo utumiaji wa dawa za kulevya na uporaji hufanyika hapo ambapo ameuagiza uongozi wa Jeshi la Polisi kushirikiana na wananchi kuhakikisha wahalifu hao wanakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria.
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia jeraha la mmoja wa wananchi wa eneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa wa Mjini Magharibi, ambaye wiki chache zilizopita alijeruhiwa na mapanga na watu wanaofanya matendo ya uhalifu katika eneo hilo.
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mjini Magharibi, ASP Suleiman Khamis Juma, akizungumza na vyombo vya habari juu ya hatua zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi kudhibiti matukio ya uhalifu katika eneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa huo, wakati wa ziara ya Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani) kutembelea maeneo sugu ya uhalifu.
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mjini Magharibi, ASP Suleiman Khamis Juma (kushoto), baada ya kutembelea eneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa huo ambalo matendo ya uhalifu ikiwepo utumiaji wa dawa za kulevya na uporaji hufanyika ambapo Katibu huyo wa NEC ameuagiza uongozi wa Jeshi la Polisi kushirikiana na wananchi kuhakikisha wahalifu hao wanakamatwa.
Mkuu
wa Polisi Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ally Kitole,
akimueleza Katibu wa Kamati Maalum ya NEC
Idara ya Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa Zanzibar, Mhandisi Hamad
Masauni baadhi ya hatua walizochukua katika kupambana na uhalifu unaoatokea
eneo la Mwanyanya Mikoroshini. Picha na Abubakari Akida
No comments:
Post a Comment