Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake Rais wa
Afrika Kusini Jacob Zuma wakati wa Nyimbo za Mataifa mawili (Tanzania na Afrika Kusini) zikipigwa katika viwanja
wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Afrika
Kusini Jacob Zuma akipita kukagua Gwaride la Heshima aliloandaliwa na Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni
wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati wakiangalia vikundi vya ngoma za
asili vilivyokuwa vikitumbuiza ndani ya viwanja vya Ikulu kwa Heshima ya ugeni
huo wa Rais wa Afrika Kusini.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mgeni wake
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kabla ya kuanza mazungumzo yao Rasmi Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni
wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati wakielekea kwenye ukumbi wa mkutano
kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya Kimaendeleo yahusuyo mataifa hayo
mawili ya Tanzania na Afrika Kusini.
Rais
wa Afrika Kusini Jacob Zuma akipunga mkono wakati akiwasili Ikulu akiwa pamoja
na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli.
Rais
wa Afrika Kusini Jacob Zuma akipunga mkono wakati akiwasili Ikulu akiwa pamoja
na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo na mgeni wake Rais wa Afrika
Kusini Jacob Zuma, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Afrika
Kusini Jacob Zuma akisoma hotuba yake wakati akizungumza na wanahabari Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru mgeni wake Rais wa
Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Rais wa Afrika
Kusini Jacob Zuma akipiga ngoma wakati alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama
Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mama Sizakele Zuma Mke wa Rais
wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kufika ofisini kwake Ikulu jijini Dar
es Salaam.
Mke wa Rais Mama
Janeth Magufuli akifurahia jambo pamoja na Mama Sizakele Zuma Mke wa Rais wa
Afrika Kusini Jacob Zuma aliyeambatana na msaidizi wake Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Vikundi vya Matarumbeta vikitoa burudani wakati Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma alipowasili Ikulu jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment