Mwenyekiti
wa Sekretarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji wa
Binaadamu, ambae pia ni Mgeni Rasmi, Adatus Magere akizungumza wakati wa
Ufunguzi wa Mafunzo ya kuzuia biashara hiyo. Kulia ni Mratibu wa Mradi wa
Shirika la Wahamiaji la Kimataifa, Tamara Keating. Mafunzo hayo yanashirikisha
wadau mbalimbali kutoka katika nchi zilizopo katika Jumuiya ya Maendeleo ya
Kusini mwa Afrika (SADC). Mafunzo hayo yanafanyika jijini Dar es Salaam.
Afisa Mkuu wa Kitengo cha Jinsia kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Dk. Joseph Pitso, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu. Wengine ni Mwenyekiti wa Sekretarieti ya kupambana na biashara hiyo, ambaye pia ni Mgeni Rasmi, Adatus Magere na Mratibu wa Mradi wa Shirika la Wahamiaji la Kimataifa nchini, Tamara Keating. Mafunzo hayo yanashirikisha wadau mbalimbali kutoka katika nchi zilizopo katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC). Mafunzo hayo yanafanyika jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mradi wa Shirika la Wahamiaji la Kimataifa nchini, Tamara Keating, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu,Wengine ni Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu,ambae pia ni Mgeni Rasmi, Adatus Magere na Afisa Mkuu wa Kitengo cha Jinsia kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Dk. Joseph Pitso . Mafunzo yanashirikisha wajumbe kutoka katika nchi zilizomo katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) hayo yanafanyika jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Binaadamu, Separatus Fella, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu yanayoshirikisha nchi zilizomo katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC). Mafunzo hayo yanafanyika jijini Dar es Salaam. Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
*********************************************
*UMASKINI WATAJWA BIASHARA HARAMU YA USAFIRISHAJI BINADAMU
Na
Mwandishi Wetu.
Hali
ngumu ya maisha ikiwepo ukosefu wa mahitaji muhimu imetajwa kama sababu kubwa
inayochochea Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu huku waaathirika wa
biashara hiyo wakiahidiwa maisha mazuri katika nchi wanazopelekwa.
Akizungumza
wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya
Usafirishaji wa Binadamu, Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Kupambana na Kuzuia
Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu (ATP), ambaye pia ni mgeni rasmi
katika mafunzo hayo, Adatus Magere amesema
wahusika wa biashara hiyo wamekua wakiwarubuni waathirika wa biashara
hiyo kuwapatia maisha mazuri na kujikuta
wakiingia katika madhara ya biashara hiyo.
Aliongeza
kuwa kuna umuhimu kwa watunga sheria na vyombo vya
sheria kutunga sheria zitakazo saidia kutokomeza kabisa biashara hiyo kwani
imekua ikiendelea kukua siku hadi siku hali inayopelekea idadi ya wahanga wa
biashara hiyo kuendelea kuongezeka.
“Tunaomba
watunga sheria na wasimamiaji wa sheria kusaidiana kwa pamoja katika kudhibiti
na kuzuia biashara hiyo kwa kutoa adhabu kali kwa wale watakaobainika kuhusika
moja kwa moja na biashara hiyo ili tatizo hili liweze kuisha katika nchi zetu,”
alisema Magere.
Aidha
Katibu Mkuu wa Sekritarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya
Usafirishaji Binadamu ambaye pia ni mwenyeji kwenye mafunzo hayo, Seperatusi
Fella, amesema kuwa ili kuweza kupambana na kuzuia biashara hiyo kuna umuhimu
kwa wadau mbaimbali kutoa elimu na mafunzo juu ya athari zitokanazo na
usafirishaji haramu wa binadamu, hivyo mafunzo ya mara kwa mara ni muhimu kwa
wananchi na wadau mbalimbali.
Naye
Mratibu wa mradi wa Shirika la Wahamiaji la Kimataifa (IOM), Tamara Keating ameahidi kushirikiana na mashirika mbalimbali
ili kukomesha biashara hiyo sambamba na kutoa elimu kwa wananchi ili kupata taarifa ya wahusika wa biashara hiyo.
Ripoti
na tafiti mbalimbali za kimataifa juu ya biashara hiyo zinaonesha Tanzania ni
mojawapo kati ya nchi nyingi zinazohuishwa na biashara haramu ya usafirishaji
binaadamu ambapo waathirika wengi wa biashara hii ni watoto walio chini ya umri
wa miaka 18 na kuendelea wanaoahidiwa
kazi nzuri na maisha mazuri pindi wafikapo katika nchi wanazopelekwa.
Mafunzo hayo yanafanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam
yakiwa na lengo la kuleta uelewa wa jinsi biashara hiyo inavyoendeshwa pamoja na
kuleta ushirikiano katika kukomesha biashara haramu ya usafirishaji binadamu
baina ya wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika.
No comments:
Post a Comment