Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista akiwa katika
ziara yake kukagua hatua za ukarabati wa nyumba za CDA zilizopo Kikuyu Dodoma
kushoto kwake ni Mkurugenzi wa CDA Mhandisi Paskasi Muragili.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
akiangalia mazingira ya nyumba za mradi wa CDA zinazoendelea kukarabatiwa kwa
ajili ya watumishi watakao hamia Dodoma awamu zijazo wakati wa ziara yake
Kikuyu Dodoma.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Mhandisi Paskasi Muragili akieleza hatua za ukarabati wa nyumba za Kikuyu kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara yake tarehe 11 Mei, 2017 Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza
jambo na Mkurugenzi wa CDA Mhandisi Paskasi Muragili wakati wa ziara yake
kukagua maendeleo ya mradi wa nyumba za Kikuyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake ya kukagua ukarabati wa
mradi wa nyumba za Kikuyu unaoendelea Mjini Dodoma. PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU- DODOMA
**************************************************
Na. Ripota Wetu, Dodoma
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu),
Jenista Mhagama amefanya ziara katika mradi wa nyumba wa Mamlaka ya Ustawishaji
Makao Makuu Dodoma ili kujiridhisha na kazi ya ukarabati inayoendelea.
Ziara hiyo ilifanyika leo Mei 11,
2017 kwa lengo la kukagua hatua zilizofikiwa na CDA ili kuhakikisha watumishi
wa Serikali wanaotarajiwa kuhamia kwa awamu zilizobaki wanaishi kwenye makazi
mazuri.
“Tunatarajia ifikapo 28 Juni, mwaka
huu CDA iwe imemaliza na kukabidhi nyumba za familia 48 kwa watumishi wa awamu
ya pili wanaotarajiwa kuhamia mwezi Julai,”Alisema Waziri Mhagama.
Aidha, Waziri Mhagama alieleza kuwa nyumba
zilizokarabatiwa awamu ya kwanza na ambazo tayari zinakaliwa na watumishi
mazingira yake ni mazuri kwani hadi hivi sasa hakuna malalamiko yoyote
aliyoyapata kutoka kwa watumishi hao.
“Hadi sasa tayari ukarabati umefikia asilimia
80 na sisi kama Serikali tunajukumu la kuisimamia CDA ili kufikia Juni mwaka
huu nyumba ziwe zimekabidhiwa zote ili kuwapa mazingira mazuri watumishi
wanaotarajiwa kuja awamu mbili zilizobaki”alisisitiza Waziri.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mamlaka
ya Ustawishaji Makao Makuu, Mhandisi. Paskasi Muragili alieleza jitihada za
ukarabati zinaendelea vizuri na zipo hatua za mwisho na tayari wameandaa
mazingira ya kugawa kazi kwa wazabuni zaidi ya mmoja ili kufikia lengo la kumaliza
ukarabati kwa wakati.
“Hadi sasa tunatarajia kupata mzabuni atakaye
shughulikia ukarabati wa nyumba 78 za awamu ya tatu na mkataba unatarajiwa
kusainiwa mwezi Juni ili kuendana na
kasi ya Serikali ya kufikia adhma yake ya kuhamia Dodoma”.Alisema Mhandisi
Muragili.
Waziri Mhagama alimalizia kwa
kusisitiza kuwa ukarabati ukamilikie kwa wakati ili ifikapo mwaka 2020 Serikali
iwe imehamia Dodoma kwa Awamu zote tatu.
“Tumeamua,tunatekeleza na
tunawahakikishia Watanzania wote ifikapo mwaka 2020 Serikali yote itakuwa
imehamia Dodoma”.Alisisitiza Waziri
No comments:
Post a Comment