Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa CCM Wilaya
ya Kinondoni Anna Angaya kulia na Katibu Nuru Mwaibako kushoto wakimkabidhi
Mwenyekiti wa kituo cha watoto yatima cha Maunga Center Zainabu Maunga baadhi
ya zawadi walizozitoa Jumuiya hiyo katika kuadhimisha wiki ya UWT. Picha na
Mariam Mziwanda
*******************************
Na Mariam Mziwanda
KATIKA
kuadhimisha wiki ya Umoja wa Wanawake UWT Wilaya ya kinondoni imekabidhi msaada
wa vifaa kwa ajili ya mahitaji mbalimbali kwa watoto yatima wa kituo cha Maunga
Center kilichopo Ananasifu Kinondoni.
Akizungumza
Mwenyekiti wa UWT Kinondoni Anna Angaya alisema Umoja huo umeona haja ya
kuwafikia watoto yatima wa kituo hicho ili kupunguza changamoto zilizopo.
Alisema UWT
inatambua kazi ya kulea watoto yatima ni ya kina mama hivyo ni wakati wa
wanawake wote kuungana na kuhakikisha majukumu ya watoto hao yanawagusa kwa
maslahi ya taifa.
“Machungu
yote yana mama sisi ndio kina mama wa CCM hatuwezi kuwaacha watoto yatima ambao
ni jukumu letu kuwaangalia, kuwasimamia na kuhakikisha wanakuwa wajenzi bora wa
taifa hili,”alisema.
Anna alisema
UWT inaamini msaada huo wa zaidi ya sh. Milioni moja utakuwa chachu kwa Jumuiya
nyingine kumuunga Mkono Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dk. John Magufuli
katika kuwafikia wananchi wa chini.
Naye
Mwenyekiti wa Kituo hicho Zainabu Maunga huku akiwa analia kwa huzuni
alishukuru CCM kwa kuguswa na maisha ya watoto hao kwakuwa wapo katika
mazingira magumu.
Alisema
kituo hicho kwa sasa kina watoto yatima 48 ambao kati yao wapo wana wazazi
mmoja mmoja na anasikitishwa na hatua ya ndugu wa watoto hao kuwatelekeza
wanapowaleta kwakuwa bado watoto hao ni wadogo wanahitaji faraja ya familia.
“Napokea
watoto hata wachanga badala ya watu kuwatupa ni bora waje waniwekee hapa nje
nikiwakuta mimi namshukuru Mungu kwakuwa mimi mwenyewe sijazaa hivyo sina mtoto
hii ni baraka kwangu lakini inapotokea pia ndugu au wazazi wa watoto wapo
wasiwatelekeze kuja tu kuwasalimia kwao ni faraja hata kama hawana
wazazi,”alisema.
Zainabu
alisema kituo hicho bado kinakabiliwa na changamoto ya vifaa vya shule,shuka za
kulalia,chakula mahali kwa ajili ya makazi kwakuwa sehemu waliyopo ni ndogo na
imetolewa kama msaada.
Alieleza
kuwa kituo hicho kimeanzishwa 2008 na kinaongozwa na lengo la elimu kwanza ili
kuwafanya watoto hao kupata haki hiyo ya msingi katika mazingira yoyote
waliyopo.
Alisema
wanaamini CCM ni chama cha wanyonge na ndio maana kimekuwa mstari wa mbele
kujali watoto yatima hivyo umadhubuti wake utaendelea kuwa imara katika
kuongoza kila chaguzi.
No comments:
Post a Comment