Habari za Punde

*5MEDIA COMPANY KUANZA KURUSHA VIPINDI TBC1


Meneja Uhusiano wa Kampuni ya 5 Media Company, Maimartha Jesse, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kuanza kazi kwa kampuni hiyo ambayo inaundwa na kumilikiwa na watangazaji na mbalimbli wa Redio na Televisheni na Watengenezaji wa vipindi vya Televisheni .
Na Sufianimafoto Reporter, jijini Dar es Salaam
KAMPUNI ya 5 Media Company ya jijini Dar es Salaam, inatarajia kuanza kurusha vipindi vyake kupitia Televisheni ya Taifa TBC1 hivi karibuni.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini leo, Menja wa kampuni hiyo, Maimartha, alisema kuwa kampuni hiyo tayari imeingia mkataba wa mwaka mmoja na Televisheni ya Taifa TBC 1 kwa ajili ya kurusha kipindi cha Afro Pop kitakachokuwa kikifanya mahojiano wanamuziki na wanamichezo mbalimbali, pamoja na watangazaji na watu maarufu.
Aidha Maimartha alisema kuwa yeye ni miongoni mwa watangazaji wa kipindi hicho, pamoja na
swahiba wake aliyekuwa nae katika kuendesha kipindi cha Afro Beat, kilichokuwa kikirushwa na Televisheni ya Chanel 5, Ben Kinyaiya.
Miongoni mwa kazi zitakazokuwa zikifanywa na Kampuni hiyo ni pamoja na kubuni na
kuandaa vipindi mbalimbali vya Televisheni, TV Programs, Kuzalisha Video za aina
zote Video Productions, Kutengeneza matangzao ya TV, Radio, Barabarani
pamoja na kusherehesha katika shughuli ama Kusimamia Matukio mbalimbali (MCs).

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.