Habari za Punde

*MBWEMBWE ZA MAONYESHO YA SABASA ZAANZA LEO DAR

*AZIM DEWJ AMWAGA MABASI YA KISASA MAONYESHO YA SABASABA
Basi hili linauzwa Sh milioni 130, linauwezo wa kubeba abiria 70 tu, na basi kubwa ya hili linauzwa Sh. milioni 150, linauwezo wa kubeba abiria 100, mabasi haya hutengenezwa na Kampuni ya Zhong Tong Bus Holding Co. Ltd, ambayo yameletwa nchini na Kampuni ya Simba Coches, na sasa mabasi haya yapo katika maonyesho ya Sabasaba ya mwaka huu katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere. Kwa mawasiliano zaidi piga No, +255222 170055, +255 774 595 00, +255752 595 00 ama Barua Pepe, altafthanki@simbatrailers.co.tz au Web Site www.simba trailers.co.tz.

Meneja Masoko wa Kampuni ya kutengeneza mabasi ya Zhong Tong Bus Ltd, Kanda ya Afrika, Mr. Li Feng, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) waliofika kwenye Banda lao katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere kwenye maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam leo na kupata maelezo jinsi mabasi hayo yanavyweza kufanya kazi kwa starehe huku kila kilichomo ndani ya mabasi hayo kikitumia umeme.

Li Feng (kushoto) na Engeneer, Hu Kuo Min, wakipozi ndani ya moja ya mabasi hayo.


Mkurugenzi Masoko wa Kampuni ya kutengeneza mabasi ya Zhong Tong Bus Ltd, Kanda ya Afrika, Engeneer, Hu Kuo Min (kushoto) akifafanua jambo kwa baadhi ya wakazi wa jijini Dar es Salaam, waliofika kwenye Banda lao katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere kwenye maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam leo.

Sehemu ya ndani ya mabasi hayo hizi ni siti za abiria kama zinavyoonekana.

Hizi ni siti za abiria katika sura tofauti.

Hii ni sehemu ya Dereva na sehemu ya kuhifadhia mizigo kwa ndani ya basi inavyoonekana.

Hili ni moja kati ya mabasi hayo linavyoonekana likiwa katika mwendo.

*WAZIRI NAGU ATEMBELEA MABANDA YA KINAMAMA MAONYESHO YA SABASABA
Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Marry Nagu (kushoto) na Mama Anna Mkapa, (wapili kushoto) wakipata maelezo ya bidhaa zinazotengenezwa na wanawake waliowezeshwa na mfuko wa Fursa sawa kwa wote ambao Mwenyekiti wake ni Mama Anna Mkapa, wakati Waziri Nagu alipotembelea banda la taasisi hiyo kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere katika maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam, leo.
"Kwa kweli bidha hizi za kina mama zinapendeza sana"
Waziri Nagu akimalizia ziara yake katika banda hilo la Kinamama.

*ULINZI WA DORIA YA ASKARI WA FARASI NDANI YA VIWANJA HIVYO
Askari Polisi akiwa katika doria ndani ya viwanja hivyo.

*MAMBO YA MAWASILIANO NDANI YA VIWANJA HIVYO NI USHINDANI, SASATEL WAINGIA KWA VITANI.
Warembo wanaofanya kazi ya matangazo ya biashara ya Kampuni ya Simu za mkononi, Sasatel, wakiwa nje ya banda lao wakisubiri na kukaribisha wateja na kuwavutia ili kutembelea katika banda hilo.

Madada hao wakipozi kivulini kupumzika kabla ya kuona Kamera ya Sufianimafoto ikiwalenga na kuamua kusimama na kuomba kupigwa tena, picha hiyo ya kwanza.

*tiGO YAKAMIA KUFANYA KUFURU MAONYESHO YA SABASABA.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu za mkononi, Tigo, kitengo cha Huduma kwa Wateja, kutoka (kushoto), Noel Nchimbi, Claudia Samwel, Doreen Muganda na Fransisca African, wakionyeshana namna ya kufanya kazi kwa haraka katika kuwahudumia wateja pindi maonyesho hayo yatakapoanza rasmi.

Mdau wa Blog ya Mtaa kwa Mtaa, Othman Michuzi, akipigwa kabari na warembo ili kuwaonyesha mafoto aliyowapiga nje ya banda hilo.

Hii ni sehemu ya ndani ya Banda hilo la Tigo ikiwa ni maalum kwa ajili ya wateja.

Othman Michuzi, akiwatungua fotoo warembo watoa huduma katika banda la Tigo, Pendo Mgonja (kulia) na Pauline Augustine.

Pendo Mgonja, akipozi katika eneo lake la kazi ndani ya banda hilo la Tigo.

Watoa huduma kitengo cha mauzo katika banda la tigo, Pauline Augustine (kushoto) na Pendo Mgonja, wakipozi kwa picha.

*HOME SHOPPING CENTER NAO WAMEJIZATITI KUTOA MALI MPYA KWA WATEJA WAO.
Hili ni banda la Home Shopping Center, linavyoonekana kwa nje...Mdau ingia ndani uone madue ya ukweli.....

Hata baadhi ya wafanyakazi wa mabanda mengine ndani ya Viwanja hivyo hufika kujionea bidhaa adimu ndani ya Banda la Home Shopping Center, hapa ni baadhi tu wakitoka ndani ya banda hilo.
*WENGINE HUPUMZIKA KIMTINDO BAADA YA KAZI NGUMU VIWANJANI HUMO
Mshkaji akiuchapa usingizi nje ya banda fulani hivi, ni baada ya kazi ngumu ya maandalizi ya mabanda hayo ya biashara......

Hebu mcheki anavyokwepa mawe duh! .......
*NI WAREMBO WA KILA AINA NDANI YA VIWANJA HIVYO
Ebwana eeh! Mdau usiniulize warembo hawa ni wa banda gani mie sijui kwa kweli wanavutia ila mie nimewafumania tu katika mitaa ya ndani ya viwanja hivo wakikatiza kwa pamoja kama hivi.....
*HUDUMA YA MSOSI KAMA KAWAIDA HAINA KUSHINDA NJAA BWANA UPENDE MWENYWE TU.
Warembo wakikatiza mitaa ya ndani ya viwanja hivyo na Plate za misosi kuwapelekea wateja wao katika mabanda, eeh ndiyo bwana Biashara matangazo na mteja ni mfalme kwa warembo hwa hata wewe hapo ulipo waagizie watakuletea tu kutoka huko walipo hadi ulipo wewe kama huamini piga namba hii 0655 306109.

*WAKOMBOZI WA WATANZANIA NIC NDANI YA MAONYESHO YA SABASABA Hili ni Bnda la Shirika la Bima la 'NIC' linavyoonekana kwa nje.

Meneja wa Bima zote kasoro magari, Ntimba Bunny (kushoto) akifafanua jambo kwa wateja wakazi wa jijini Dar es Salaam waliotembelea Banda hilo katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo mchana, katika maonyesho ya Sabasaba.

Kutoka (kushoto) ni Meneja Masoko wa Shirika hilo, Henry Machoke, Meneja Uhusiano na Mawasiliano, Mwanaidi Shemweta, Ofisa Masoko Mwandamizi, Adelaida Muganyizi na Meneja wa Bima Zote kasori za Magari, Ntimba Bunny, wakipozi kwa picha ndani ya Banda lao baada ya majaji kupita na kukagua banda hilo leo mchana.

Wahudumu wakijipanga tayari kwa kazi ndani ya banda hilo.



Banaz na Bloshua za NIC ndani ya banda hilo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.