Habari za Punde

*JAMANI BIASHARA NI POPOTE SI LAZIMA NDANI YA SABASABA

"Hata Hapa inafaa wakiona ndani bei kubwa watakuja weeeenyeweeee" Mfanyabiashara wa chakula 'Mama Lishe' akimhudumia mteja wake kwa kumpimia sahani ya ubwabwa, akiwa pembezoni mwa barabara nje ya Viwanja vya Sabasaba, kama alivyonaswa na Kamera ya Sufianimafoto na hii inaonyesha ni jinsi gani wafanyabiashara wadogo wanashindwa kumudu gharama za ushuru ili kujenga mabanda ndani ya viwanja hivyo na pia inaonekana kuwa bei ya vyakula ndani ya viwanja hivyo ni ghari kiasi cha kuwashinda baadhi ya wafanyakazi wa mabanda na kuamua kutoka nje ili kutafuta angalau bei nafuu kama unavyomcheki jamaa huyu ikionekana kamba ya kitambulisho shingoni alitoka ndani na kuja eneo hili kujisevia.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.