Habari za Punde

*ASKARI WA USALAMA BARABARANI WAPEWA MAFUNZO YA KUTUMIA MFUMO WA KUDHIBITI MWENDO WA MABASI

Mwenyekiti wa Chama cha Wenye Mabasi (TABOA), Mohamed Abdallah (wapili kushoto) waliosimama, akiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi wa 'It Support Team' waliokuwa wakitoa mafunzi kwa askari wa usalama barabarani, kuhusu mfumo wa kusimamia mwendo wa magari, madereva na abiria utakaokuwa katika 'Systeam' utakaomwezesha askari kumuona dereva ma gari lolote na popote litakapokuwapo iwapo litakuwa tayari limekwishaingizwa kwenye mfumo huo. Mafunzo hayo yalianza jumatatu na yanatarajia kumalizika kesho kwenye Ofisi za Polisi Makao makuu ya Trafik jijini Dar es Salaam, ambapo utazinduliwa rasmi hapo kesho.

Mwendesha mafunzo ambaye pia bi Meneja wa It kutoka Kampuni ya uTRACK, Richard Kimani, akiwaelekeza jambo baadhi ya askari wa usalama barabarani, wakati wa mafunzo ya jinsi ya kusimamia mfumo wa mwendo wa magari na madereva barabarani na abiria, kuwa katika mfumo maalum, ambapo wenye mabasi makubwa watakaohitaji huduma hiyo watahitaji kusajiliwa ili kuonekana katika ‘System’. Mafunzo hayo yalianza Julai 28 na yanatarajia kumalizika kesho katika Kituo cha Polisi Makao makuu ya Trafiki.

Maafande kutoka (kulia) ni Coplo. Muhidin Mohamed, Coplo. Erwin Mahundi na Coplo. Flora Mashishanga, wakiwa bize kujifunza mfumo huo katika Kompyuta, wakati wa mafunzo hayo.



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.