Habari za Punde

*NDANI YA VIWANJA VYA SABASABA LEO, MAONYESHO KUFUNGULIWA KESHO NA JUMA MWAPACHU

Katibu Twala wa Wilaya ya Temeke, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Tan Trade, Ellyn Mcha, akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za viwanja hivyo leo mchana kuhusu, ufunguzi wa maonyesho ya 34 ya Biashara ya Kimataifa yanayofunguliwa kesho na Katibu Mkuu wa Afrika Mashariki, Balozi Juma Mwapachu, ambapo alisema kuwa ufunguzi huo unatarajiwa kufanywa mida ya saa sita mchana.
*AKAZI WA JIJINI DAR WAANZA KUJISEVIA MAHITAJI KATIKA MAONYESHO HAYO
Wakazi wa jijini Dar es Salaam, wakitoka kwenye viwanja vya mwalimu Nyerere na vyombo walivyonunua katika maonyesho hayo yanayoendelea, ambapo yanatarajiwa kufunguliwa rasmi hapo kesho.

*NDA LA BUNGE KATIKA MAONYESHO YA 34 BISHARA YA KIMATAIFA MBONA LIMEDOROLA?
Katika Viwanja hivyo kumekuwa na mabanda mengi ya biashara, mengine yakiwa yameingia kwa mara ya kwanza na mengine ni makongwe, lakini katika Banda hili hadi hii leo ambapo imebaki siku moja tu kufunguliwa kwa maonyesho hayo, bado limepooza namna hii kulikoni? ama ni kwa sababu Waheshimiwa wote bado wapo huko mjengoni nini? ama ni ubize na mawazo yte bado yapo katika naniliu za kurudisha fomu hukoooo, Dom?

Ebwana eeh! Banda hili kwakweli linavutia kiaina lakini mbona bado naniliu?????
*WAREMBO WA UTALII WAVUTIA WATEJA KATIKA MAONYESHO YA SABASABA DAR
Warembo Marry Nguma (kulia) na Grace Lucas, wanaotarajia kushiriki katika kinyang'anyiro cha kumsaka mrembo wa Utalii wa Taifa wa mwaka 2010-2011, wakiwa katika Banda la kuuza vipodozi na dawa, wakitoa maelezo kwa mteja aliyefika katika banda hilo la Makai Moringa (Mlonge). Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo ya Makai Moringa Enterprises, Eileen Kasubi.
Kutoka (kushoto) ni Edina Andrew, Latifah Bakari na Pendo Ernest wakiwa katika banda jingine la vitu asilia wakipanga na kusubiri wateja.

Mrembo wa utalii wa mkoa wa Dar es Salaam, Sophia Dio, akimwelekeza mteja jinsi ya kutumia dawa iliyotengenezwa kwa mitishamba, wakati wa maonyesho ya 34 ya Biashara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini.
*MSOSI HAUNA USISTA DU BWANA NI POPOTE TU
Ukimcheki ni Sister Du waukweli, ambaye huwezifikiri kuwa ungeweza kumkuta akila ama kujisevia msosi katika eneo la wazi kama hivi ambalo halikukaa rasmi kwa ajili ya suala hilo, lakini ndivyo ilivyo Mdada huyu alikuwa katika banda lake la biashara ambalo lilijaa wateja muda wote na ili aweze kulitendea haki tumbo ilimbidi kutoka nje na kujificha mahala hapa nyuma ya banda ambapo ni njiani kabisa wanapopita watu ili aweze kula kwa raha, na baada ya kuona kamera ya Sufianimafoto ikimnyemelea kwa kweli hata hamu ya msosi ilimwishia na hakuweza kula tena kwa raha, lakini ndiyo kazi na haka kamera hii ilikuwa kazini hivyo twende sawa.
*SHIKAJI AKIWACHORA WATOTO USONI
Mchoraji aliyejitambulisha kwa jina la Edward Martine, akiwachora watoto vijikatuni katika paji za uso kama alivyokutwa na Kamera ya Sufianimafoto, kwenye Viwanja vya Sabasaba leo mchana, huku wengine wakiwa wamepanga foleni kusubiri huduma hiyo.









No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.