*BAISKELI NA LUMBESA KAMA PICK UP
Baiskeli ikiwa imebeba mzigo kiasi cha kuizidi uwezo na mzigo huo ukioonekana kuwa na uzito mkubwa kiasi cha kuweza kubebwa na gari, lakini waswahili husema kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake na Mtaji wa Masikini ni Nguvu zake mwenyewe, hivyo kidume hiki mpaka hapo kinaonekana kufaulu usemi huo wote kama anavyoonekana alivyokutwa na Kamera ya Sufianimafoto katika mitaa ya Posta jijini Dar es Salaam, akielekea kuvuka Pantoni kupeleka kwa wateja wake kutoka Sokoni Kariakoo leo mchana.
*WAANDISHI WA HABARI WAKISUBIRI STORI JE ZITAKUJA?

Jamani enyi wanafunzi mnaotoka Vyuoni na kujiunga na vyombo mbalimbali ili kufanya Fild, hebu jitahidini basi kujishughulisha msizani kuwa stori ama habari hupatikana Idara ya Habari Maelezo pekee, kwani unapokuwa na stori zaidi ya zinazopatikana mahala hapo yaani zile unazozihangaikia zaidi kuliko za mezani hamjui kuwa ndizo hasa zinaweza kukupeni Credit???, Hebu jihangaisheni jamani basi msibweteke namna hiyo.....
*DALADA NA MAFUTA YA KIDEBE WAPI NA WAPI

Dereva wa gari la abiria linalofanya safari zake Temeke Sinza, akiweka mafuta katika gari lake baada ya gari hilo kuzimika ghafla katika barabara ya Tandale Dar es salaam huku likiwa na abiria na kuwachelewesha abiria hao kwa muda mrefu wakati kondakta wa gari hilo alipokimbia na kidumu kununua mafuta kwenye Kituo cha BP kilichopo Sinza Kijiweni, hebu pima umbari huo ewe mwenyeji wa dar na kisha fikilia ni jinsi gani abiria haoa walicheleweshwa mahala hapo. MADREVA ACHENI KUWEKA LITA TANO TANO........
No comments:
Post a Comment