
Wanachama wa CUF, wakiandamana na mabango kumsindikiza Mgombea urais wa Chama hicho Ibrahim Lipumba kurudisha fomu katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Taifa Jijini Dar Es Salaam leo mchana. Wanachama hao waliandamana kuanzia kwenye Ofisi za CUF zilizopo Buguruni hadi katika ofisi hizo huku wakiwa na mabango na msafara wa waendesha pikipiki.

Mkereketwa wa chama cha CUF ambaye hakufahamika jina leke, ambaye ni mlemavu akivuka barabara wakati wa maandamano hayo, ambaye pia alikuwa ni mmoja kati ya wanachama hao waliotembea kwa miguu kutoka Buguruni hadi Posta kumsindikiza Lipumba.

Hawa ni sehemu tu ya umati wa watu waliojumuika kumsindikiza Lipumba.
No comments:
Post a Comment