Habari za Punde

*MADEGA AKABIDHI OFISI RASMI KWA LLOYD

Mwenyekiti wa Yanga aliyemaliza muda wake, Imani Madega (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhiana ofisi leo mchana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Lloyd Nchunga.

Imani Madega akiweka saini katika Nyaraka hizo kabla ya kuukabidhi uongozi mpya wa Klabu hiyo leo, wakati wa hafla ya kukabidhiana ofisi iliyofanyika kwenye Jengo la Klabu hiyo mtaa wa Jangwani.

Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga ya Jijini Dar es Salaam, aliyemaliza muda wake, Imani Madega (katikati) akimkabidhi nyaraka za ofisi Mwenyekiti mpya wa Klabu hiyo, Lloyd Nchunga, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi ofisi iliyofanyika kwenye Klabu hiyo mtaa wa Jangwani na Twiga jijini leo mchana. Kulia ni Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Lawrance Mwalusako.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.