Habari za Punde

*MARIGA ASHINDWA KUTEMA CHECHE KWA STARS

Kiungo mshambuliaji wa Timu ya Harambee Stars ya Kenya, Macdonald Mariga (kushoto) akidhibitiwa na wachezaji wa Taifa Stars, Jerry Tegete (katikati) na Nurdin Bakari, wakati wa mchezo wa Kimataifa wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam leo jioni. Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.


Beki wa timu ya Taifa (Taifa Stars) Kelvin Yondan (kulia) akichuna kuwania mpira na mshambuliaji wa Harambee Stars, John Barasa, wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru.
Kipa wa Taifa Stars, Shaban Kado, akiokoa shuti lililopigwa na Dennis Oliech wa Harambee Stars wakati wa mchezo huo.

Wachezaji wa Taifa Stars, wakimpongeza Mrisho Ngassa, baada ya kuipatia timu yake bao la kusawazisha katika kipindi cha pili cha mchezo baada ya kumtoka beki na kumchungulia Kipa wa Harambee Stars Wilson Obungu aliyejaribu kutokea ili kuokoa na kupishana na mpira na kufanya matokeo kuwa 1-1.

Mariga akikosa bao na kuanguka langoni mwa Stars.





No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.