Mshambuliaji wa Simba Mohamed Banka (kulia) akimtoka beki wa African Lyon, Aziz Sibo, wakati wa mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Vodaco Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, ambapo Simba iliibuka kidedea kwa kuwatandika bila hurua wadogo zao hao kwa mabao 2-0. huku mabao yote yaifungwa na Amir Maftah, hadi mwisho, SIMBA 2-AFRICAN LYON 0. Nayo Yanga ya Dar es Salaam pia leo ilishuka katika Dimba la Jamhuri mjini Dodoma kuwakabili Maafande wa mji hu Polisi Dodoma, ambapo Yanga imeshinda bao 1-0 huku bqqo hilo likifungwa na Jerry Tegete. YANGA 1-POLISI DODOMA 0. Kagera Sugar ilikuwa katika Dimba la nyumbani Kaitaba mjini Bukoba mkoa wa Kagera, ikimenyana na Ruvu Shooting, ambapo katika mchezo huo Kagera Sugar imeshindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani kwa kuchapwa bao 1-0. KAGERA SUGAR 0-RUVU SHOOTING 1. Nayo Azam Fc, ilikuwa ugenini katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha ikimenyana na AFC ya mjini humo, ambapo imeweza kuibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 2-0, huku mabao yote yakiwekwa kimiani na John Boko. AFC ARUSHA 0-AZAM FC 2.Toto Africa ilikuwa katika uwanja wa nyumbani Kirumba ikichuana vilivyo na JKT Ruvu, ambapo imeweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0. TOTO AFRICA 1-JKT RUVU 0. Majimaji ya Songea ilikuwa ikiwakaribisha wana wa sukari Mtibwa Suga katika Uwanja wa Sokoine na kushindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani ambapo imetolewa nishai kwa kuchapwa bao 1-0, huku bao hilo likifungwa na Zubeir Katwila. MAJIMAJI 0-MTIBWA SUGAR 1.
Hii ndiyo faulo iliyopelekea Simba kupata penati katika kipindi cha pili, Nico Nyagawa akijirusha ndani ya penati Boksi baada ya kuvaana na Kipa wa A. Lyon, Ivo Mapunda (aliyeanguka chini)

Kipa wa African Lyon, Ivo Mapunda akipishana na mpira uliopigwa na Beki wa kushoto wa Simba Amir Maftah kwa penati.
No comments:
Post a Comment