Habari za Punde

*TIGI YAKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA 'JIKOKI'

Ofisa Viwango wa tigo, David Zacharia , akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi la kukabidhi zawadi za washindi Promosheni ya JIKOKI iliyofanyika kwenye Ofisi za Tigo Makao Makuu jijini Dar es Salaam leo mchana. Kushoto ni Meneja Matangazo wa Kampuni hiyo, Redemtus Masanja.

Meneja Matangazo wa kampuni ya Simu za mkononi Tigo, Redemtus Masanja (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh milioni 2, simu aina ya Brack Berry na Lap Top ya Accer, mshindi wa Promosheni ya ‘JIKOKI, Watambile Chisagimbi, mkazi wa Tabata Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa Promosheni hiyo iliyofanyika jijini . Katikati ni Ofisa Viwango wa Tigo, David Zacharia.

Meneja Matangazo wa kampuni ya Simu za mkononi Tigo, Redemtus Masanja (kushoto) akimkabidhi zawadi ya simu aina ya Brack Berry, mshindi wa Promosheni ya ‘JIKOKI, Irene James mkazi wa Kimara Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa Promosheni hiyo iliyofanyika jijini

Mshindi akiwa na zawadi yake ya Lap Top ya Accer
Mshindi wa bajaji, Idd (kushoto) akiwa na maofisa wa tigo mara baada ya kukabidhiwa.



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.